Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi: Kila nitakayemteua atawajibika kutimiza majukumu yake

Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi: Kila nitakayemteua atawajibika kutimiza majukumu yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya 8 ni kukuza uchumi katika Nyanja zote ili kuwapa vizuri wafanyakazi wake .

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wafanyakazi huko katika ukumbi wa Shehe Idrisa Abdul wakili Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Dkt. Hussein amesema katika uongozi wake atajenga mawasiliano baina yake na wafanyakazi wote ili kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.

“kuweni na imani na matumaini makubwa na mimi kwani nina nia njema na Zanzibar na kila siku namuomba Mungu anisaidie kwa hili na nitatimiza ahadi yangu kwenu kwani ahadi ni deni “

Aidha Dkt. Huseein amesema hatakuwa na muhali wala huruma kwa wabadhirifu na walarushwa katika Serikali yake na atahakikiha kila mtu atakaemchagua anawajibika na kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Hata hivyo mgombea huyo amewakata wafanyakazi hao kukichagua chama cha mapinduzi CCM katika ngazi zote ili atekeze ahadi alizowaahidi.
 
wagombea wengine na wao wana haki ya kuzungumza na wafanyakazi kwenye vikao rasmi?
 
Hahaha yeye kateuliwa kawajibika lini na wapi?!
Zanzibar inawenyewe.
 
Hivi jamani ni mimi tu au na nyie mna share mawazo yangu. Huyu mtu hana mvuto wa kisiasa kabisa. Kapoozaaa. Yaani ni ile baba kaingia siasa na mi naingia.

Akiongea nusu saa waweza sinzia kabisa. Kuhusu utendaji wake sina uhakika maana wizara yake ya ulinzi alikua yupo hata hatumsikii kivile
 
Hao ambao hawana maneno mengi, wana vitendo vinavyo wasemea. Madebe shinda kama Lissu ndio wale waliofananishwa na mbwa kukimbiza gari, akibweka! Lakini gari ikisimama mbwa hana cha kuifanya!
 
Hao ambao hawana maneno mengi, wana vitendo vinavyo wasemea. Madebe shinda kama Lissu ndio wale waliofananishwa na mbwa kukimbiza gari, akibweka! Lakini gari ikisimama mbwa hana cha kuifanya!

Sipingi ulichoongea ila nna wasiwasi sana huyu jamaa ni kwamba system imembeba.

Imagine system ingewabeba kina Madaraka na Makongoro. Huenda tungesifia ulevi wao kwamba walevi ndio wanapanga mipango madhubuti.
 
Aanze kurudisha yale mashamba ya watu aliyokupua baba yake kule Kitope na pia amwambie Magufuli yale mashamba ya watu aliyokupua baba yake kule Morogoro ayarudishe
 
Wazanzibari CCM walishaikataa tangu tuingie mfumo wa vyama vingi! Huku kuendelea kuwang'ang'aniza kuongozwa na chama wasichokipenda na watu wasio wachagua ndiko kunakoididimiza Zanzibar!
 
Mwenye ile video clip inamuonesha mama wa Kizanzibari anayesema hawawezi kukabidhi nchi kwa sanduku la la kura, aiweke hapa
 
Husein Mwinyi Rais wa Zanzibar ajae Inshallah, hana skendo chafu na huwa ni mtu mchapakazi kweRi kweRi.
 
Yaani nisubiri aibu ya Zenji, sijui safari hii wanakusudia kufanya nini na matokeo, yaani tacheka sana,sababu yaliyolalamikiwa hapo mwanzo ni kutangazwa asie shinda, kufutwa kwa matokeo, kuibwa kura, nasubiri picha lifuatalo, na lazima litakuwepo!
 
Husein Mwinyi Rais wa Zanzibar ajae Inshallah, hana skendo chafu na huwa ni mtu mchapakazi kweRi kweRi.

Huyo anayempigia kampeni Seif Ali Idi ana nyumba zaidi ya 37 amekupua ardhi za watu na juzi kafungua jumba lake jengine huku Pemba , Aanze kwanza kumwajibisha yeye , kama anao ubavu, kwa kumkataa kwenye kampeni zake

Mwenye ile video clip inamuonesha mama wa Kizanzibari anayesema hawawezi kukabidhi nchi kwa sanduku la la kura, aiweke hapa
We ya nini? Achana na hiyo video, muhusika ameshafariki mwache apumzike huko aliko.
 
Huyo anayempigia kampeni Seif Ali Idi ana nyumba zaidi ya 37 amekupua ardhi za watu na juzi kafungua jumba lake jengine huku Pemba , Aanze kwanza kumwajibisha yeye , kama anao ubavu, kwa kumkataa kwenye kampeni zake

Dr.Hussein Mwinyi hana skendo,endelea kuzitafuta ukizipata kisha uzilete hapa kwa fact na ushahidi.
 
Back
Top Bottom