Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi: Kila nitakayemteua atawajibika kutimiza majukumu yake

Zanzibar 2020 Dkt. Mwinyi: Kila nitakayemteua atawajibika kutimiza majukumu yake

Ukizipata za Dr.Hussein Mwinyi zitupie hapa kwa ushahidi.

Humo alimo CCM si mumejaa scandal na yeye akiwa waziri wa ulinzi . Hivi ule uchaguzi uliopita na wale wanajeshi waliovamia kituo cha ZEC walikuwa wa wapi ?
 
Humo alimo CCM si mumejaa scandal na yeye akiwa waziri wa ulinzi . Hivi ule uchaguzi uliopita na wale wanajeshi waliovamia kituo cha ZEC walikuwa wa wapi ?
Zitafute skendo za Dr.Hussein Mwinyi kisha uzilete kwa fact na ushahidi.
 
Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya 8 ni kukuza uchumi katika Nyanja zote ili kuwapa vizuri wafanyakazi wake .

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wafanyakazi huko katika ukumbi wa Shehe Idrisa Abdul wakili Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Dkt. Hussein amesema katika uongozi wake atajenga mawasiliano baina yake na wafanyakazi wote ili kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.

“kuweni na imani na matumaini makubwa na mimi kwani nina nia njema na Zanzibar na kila siku namuomba Mungu anisaidie kwa hili na nitatimiza ahadi yangu kwenu kwani ahadi ni deni “

Aidha Dkt. Huseein amesema hatakuwa na muhali wala huruma kwa wabadhirifu na walarushwa katika Serikali yake na atahakikiha kila mtu atakaemchagua anawajibika na kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Hata hivyo mgombea huyo amewakata wafanyakazi hao kukichagua chama cha mapinduzi CCM katika ngazi zote ili atekeze ahadi alizowaahidi.
Kamwe hutakuwa Rais wa Zanzibar.
 
Sawa raisi wa kuteuliwa, tumekusikia.
Ngumu sana kuwajibisha mibuyu ya Chama.

Everyday is Saturday................................😎
 
Zitafute skendo za Dr.Hussein Mwinyi kisha uzilete kwa fact na ushahidi.

Hivi ule uchaguzi uliopita na wale wanajeshi waliovamia kituo cha ZEC walikuwa wa wapi ? Yeye akiwa nani wakati huo ??
 
kaongea na wafanyakazi kama nani? wafanyakazi wa wapi? heeee jamaniiiii
 
Back
Top Bottom