GE2025 Dkt. Mwinyi kuja na mpango wa uwekezaji mkubwa hoteli ya Bwawani

GE2025 Dkt. Mwinyi kuja na mpango wa uwekezaji mkubwa hoteli ya Bwawani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi endapo atapewa tena ridhaa ya kuongoza Zanzibar kushirikisha sekta binafsi kuja na uwekezaji Mkubwa katika eneo la Bwawani ili kuchochea hadhi ya eneo hilo na uchumi wa Zanzibar

Dkt. Mwinyi ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Malindi ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake kueleka Uchaguzi Mkuu wa oktoba 2025

Dkt Mwinyi amesema katika eneo hilo lenye historia kubwa na thamani kwa uchumi wa Zanzibar hayuko tayari kuja na mpango wa uwekezaji wa fedha kidogo bali anahitaji uwekezaji mkubwa utakaochochea uchumi wa Zanzibar na kutoa fursa kubwa za ajira kwa vijana.

 
Back
Top Bottom