GE2025 Dkt. Mwinyi na Mkewe wasimama njiani kununua mabungo wakitoka kwenye Kampeni Wete

GE2025 Dkt. Mwinyi na Mkewe wasimama njiani kununua mabungo wakitoka kwenye Kampeni Wete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwa ameambatana na Mke wake , wamesimama njiani kununua matunda aina ya Mabungo wakitokea Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya mkutano wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), katika mwendelezo wa Kampeni zake.

1759923334535.png
Tukio hilo limevutia hisia za Wananchi waliokuwa kandokando ya Barabara, ambapo wengi walionesha furaha na kupongeza unyenyekevu wa Viongozi hao, waliokuwa wakijumuika nao katika shughuli za kawaida za maisha ya kila Siku.

1759923343688.png

1759923355685.png

1759923375228.png
 
Mwinyi ni miongoni mwa watu ninaowakubali sana.

Nilitamani angekuja kuwa kiongozi wa Tz angesaidia jambo.

Ila siasa za namna hii kama anapitia JF basi aachane nazo.
 
Back
Top Bottom