Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema chama hicho kitaendelea kusimamia na kulinda misingi ya amani, umoja na mshikamano ambayo imeiwezesha Zanzibar kufikia mafanikio makubwa ya maendeleo katika miaka mitano iliyopita.
Akizungumza leo, Alhamisi Oktoba 16, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Paje, mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Mwinyi amesema sera kuu ya Chama Cha Mapinduzi imejikita katika kudumisha misingi hiyo mikuu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa.
“Mpaka sasa hivi katika miaka mitano iliyopita tumekwenda vizuri, nchi yetu ina amani, ina umoja, mshikamano, na hata tuna maridhiano ya kisiasa. Hii imesababisha mambo mengi ya kimaendeleo kufanyika kwa sababu ya amani tuliyokuwa nayo,” amesema.