GE2025 Dkt Mwinyi: Nchi yetu ina amani, ina umoja, mshikamano, na hata tuna maridhiano ya kisiasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema chama hicho kitaendelea kusimamia na kulinda misingi ya amani, umoja na mshikamano ambayo imeiwezesha Zanzibar kufikia mafanikio makubwa ya maendeleo katika miaka mitano iliyopita.

Akizungumza leo, Alhamisi Oktoba 16, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Paje, mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Mwinyi amesema sera kuu ya Chama Cha Mapinduzi imejikita katika kudumisha misingi hiyo mikuu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa.

β€œMpaka sasa hivi katika miaka mitano iliyopita tumekwenda vizuri, nchi yetu ina amani, ina umoja, mshikamano, na hata tuna maridhiano ya kisiasa. Hii imesababisha mambo mengi ya kimaendeleo kufanyika kwa sababu ya amani tuliyokuwa nayo,” amesema.

Your browser is not able to display this video.
 
..jina lake kwa usahihi ni Dr. Husseni Nzasa Chande Magandi. Ni Mtanganyika.
 
Nchi yao! Acha na sisi tupambanie nchi yetu Tanganyika βœŒπŸΏπŸ’—πŸ’—πŸ’—πŸ’—
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…