GE2025 Dkt. Mwinyi: Nitaifanya Tumbatu kuwa Wilaya

GE2025 Dkt. Mwinyi: Nitaifanya Tumbatu kuwa Wilaya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi wananchi wa kisiwa cha Tumbatu katika miaka mitano ijayo atahakikisha anaifanya kisiwa hicho kuwa wilaya.

1759582527010.png
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni unaofanyika kisiwa cha Tumbatu kilichopo wilaya ya Kaskazini ‘A’ mkoa wa Kaskazini Unguja.

Fahamu kuhusu > Kaskazini Unguja: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Mkuu 2025

Dkt. Mwinyi amesema kuna wakati wakazi wa kisiwa cha Tumbatu walimuomba kuifanya kisiwa hicho kidogo kuwa wilaya kamili na kwamba anawahakikishia ataifanya hivyo kipindi kijacho.

"Sasa ni wakati Tumbatu kuwa wilaya kamili kuna kipindi tuliitaka wizara husika waanze mchakato wakulifikisha hilo wakaniambia kuna vigezo lazima vitimie na kwamba ahaadi yenu kwenu ni kipindi kijacho tutaongeza wilaya na kuifanya iwe wilaya kamili"
 
Back
Top Bottom