Dkt. Mwinyi: Serikali kujenga nyumba 5,000 za makazi unguja na pemba ndani ya miaka mitano

Joined
May 2, 2026
Posts
64
Reaction score
55
DKT. MWINYI: SMZ KUJENGA NYUMBA 5,000 ZA MAKAZI UNGUJA NA PEMBA NDANI YA MIAKA MITANO

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inakusudia kujenga nyumba 5,000 za makaazi kwa wananchi wa Unguja na Pemba ndani ya kipindi cha miaka mitano kupitia Shirika la Nyumba la Zanzibar(ZHC).

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 13 Mei 2026, katika mkutano maalum wa kutoa shukrani kwa wanachama wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema Serikali imeweka mkazo katika ujenzi wa nyumba za kisasa ili kuwaondoa wananchi wanaoishi katika nyumba chakavu na zisizo salama, huku akibainisha kuwa baadhi ya nyumba zilizojengwa zaidi ya miaka 62 baada ya Mapinduzi zinahitaji kufanyiwa maboresho au kujengwa upya.

Soma Pia: Mwinyi: Serikali imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu na ustawi wa wananchi wa Unguja na Pemba

Aidha, Dkt. Mwinyi amewahimiza wanachama wa CCM kuendelea kuimarisha Chama kwa kudumisha mshikamano, kurejesha madarasa ya itikadi na kuanzisha miradi ya kiuchumi yenye tija katika wilaya na mikoa.

Ziara ya kutoa shukrani kwa wanachama baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 imehitimishwa leo Kisiwani Pemba baada ya kuanza rasmi tarehe 09 Mei 2026.
 
CCM inaahidi na kutekeleza,

well done Dr Hussain Ali Mwinyi.
unafanya kazi nzuri sana Baba,

God bless you 🔥
 
Back
Top Bottom