Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi uungwana wako wa hoja ni sharti ukupeleke Ikulu, Sijaona mpinzani mbadala dhidi yako

Uchaguzi 2020 Dkt. Mwinyi uungwana wako wa hoja ni sharti ukupeleke Ikulu, Sijaona mpinzani mbadala dhidi yako

Deogratias Mutungi

Senior Member
Joined
Oct 1, 2019
Posts
140
Reaction score
181
Dkt. Mwinyi mgombea wa kiti cha urais Zanzibar ni kiongozi mwenye hoja mama na falsafa za ukombozi zenye kujikita kwenye uungwana wa utu kwanza katika kuwatumikia watu, anashawishi anapojenga hoja na ana jenga hoja zenye mwelekeo wa sura za kiutumishi kwa Wazanzibar, ni viongozi wachache wenye kariba kama ya Dkt. Hussein Mwinyi, Kwa sasa hoja za Mwinyi ni ramani mpya ya mafanikio kwa Wazanzibar.

Kwa mantiki ya kiutafiti wa kawaida Dkt. Mwinyi hana mpinzani na ndiye rais mtarajiwa wa Zanzibar kwa sababu kiongozi imara na shupavu upimwa kwa hoja zenye mwelekeo wa kukomboa watu na kutatua kero zao kiuchumi, Mwl. Nyerere alifanya hivyo wakati anajenga hoja za kuwapigania Watanganyika na hatimaye uhuru ukapatikana, Dkt. Mwinyi anafanya hivyo kwa weledi mkubwa mithili ya Mwl. Nyerere, Wazanzibar tunayo haki na wajibu wa kumchagua kwa wingi Dkt. Hussein Mwinyi hapo Oktoba 28, hiki ni chuma cha pua chenye udhubutu na falsafa pekee za uwajibikaji kwa watu tusifanye kosa tusije tukajuta hpo badae.
.
Hoja za Upinzani zinakubalika lakini zina mapungufu ya kimantiki hivyo ni ngumu kwa sasa kuwapa mamlaka ya kushika dola, tuwape muda wajipange bila shaka wakati ukifika watapewa dola, Kwa sasa tumpe kijana mwema na mjenga hoja za kimapinduzi katika mrengo wa kuwatumikia Wazanzibar, ni fursa adimu hii tuitumia kwa umakini tusikosee na tusije tukajutia, Mbele ya Dkt. Mwinyi naiona Zanzibar angavu, mpya na yenye mwelekeo wa kiuchumi na amani imara.
 
hivi ni huyu ndiye zenji wanamwita mwinyi mpeku???
 
Back
Top Bottom