ni sahihi, dini haijawahi kuokoa roho, pamoja na kwamba, as a matter of fact, ni ya muhimu kwa mambo ya kidunia kama ushirika na wenzako, kusaidiana katika matatizo, na kutukumbuka kufanya mema, ni platform tu ya kutukumbusha kufanya hivyo. however, hata kama tukikumbushwa hatuwezi kuishinda dhambi bila kuwezeshwa na Nguvu za Mungu, dini peke yake kama mfumo uliowekwa na wanadamu namna ya kumwendea Mungu haiwezi kukuokoa. Unahitaji personal relationship with God, a very personal one.
kwa wale ambao bado, unatakiwa kumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, uokoke manake, na umwombe Mungu akupe Roho Mtakatifu akusaidie katika maombi na kukuongoza kuishinda dhambi. Hii ni kwasababu, hata kama tunakuwa na dini, lakini hatufuati dini basi Neno la Mungu, Neno la Mungu kwanza na mapokeo ya dini baadaye kama yanaendana na Neno.
kwenu ninyi mnaoamini kuondoka kwenye dini moja ni dhambi, jueni kuwa hata Mungu hizo dini zenu hazitambui, anamtambua Yesu Kristo tu kama kafara, mfano, wewe mkatoliki tukisema okoka hiyo dini ya ukatoliki haiokoi ila Yesu anaokoa, au wewe mlutheran, mumorovian au angalican au muislam, tukisema acheni kufuat amapokeo ya wanadamu yasiyo ndani ya Neno la Mungu, msifikiri kuiacha dini yenu ni dhambi, hapana, dini haimfikishi mtu mbinguni, ila Wokovu ndani ya Yesu Kristo.
hata walokole (ambako mimi nipo TAG, EAGT, PENTECOSTS n.k), kama upo huku lakini matendo yako ni machafu usifikiri kuwepo ndani ya dini kutakuokoa, never. Mungu anaangalia roho, na hadanganyiki.