Dkt. Nchemba: Ukwepaji wa kodi liwe jambo la aibu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ipo haja kwa watoto wadogo kuanza kuelimishwa juu ya umuhimu wa kulipa kodi ili watoto wakue wakijua kwamba ukwepaji wa kodi ama upokeaji na utoaji wa rushwa ni jambo la aibu katika familia.

MWIGULUU%2011.jpg

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo ameitoa leo Juni 24, 2021, Bungeni Dodoma na kuongeza kuwa taifa litakalojengwa na watu wa aina hiyo litakuwa ni bora zaidi na kwamba jamii ya sasa haijafikia hatua ya watu kuonashida kujihusisha na masuala ya rushwa na na ukwepaji wa kodi.

"Tumeendelea kuongea na wenzetu wa Wizara ya Elimu kwamba tunakijenga vipi kizazi cha nchi yetu tangu wakiwa wadogo waelewe masuala ya wajibu, kodi na kupinga rushwa, watoto wetu tukiwaambia tangu wadogo wakaanza kuona ni aibu kukamatwa kwenye masuala ya kukwepa kodi, tangu wapo shuleni wakaanza kuona ukionekana unakwepa kodi ama rushwa ni jambo la aibu kwenye familia yenu Taifa litakalojengwa na kizazi cha aina hicho ni bora sana," amesema Dkt. Nchemba.
 
Hapa wakitaka kufanikiwa kwanza kuwe na usawa katika ulaji wa keki ya Taifa. Yeye anaepokea 25M ni rahisi sana kusema ila mtu anayepokea 500K kwa mwezi halafu 2M imekuja karibu yake anaanzaje kuiacha.

Kwanza waondoe ukoloni mamboleo then watafanikiwa kwa urahisi zaidi.
 
Kodi ulipe Hospitali hakuna Dawa Wabunge feki wanachezea pesa Upigaji wa kiwango nk
 
Elimu ya kodi iendane sambamba na utoaji haki kwa raia wote bila ubaguzi, raia aweze kuhoji mapato na matumizi ya serikali yake na isiwe ni uchochezi - kwa mfano mtu ukihoji kwa nini mamilioni yanalipwa kwa wabunge ambao hawana vyama utaitwa mchochezi - hapa ndipo tatizo lilipo.

Ruhusuni taasisi za nje na ndani zilizokuwa zinatoa elimu ya uraia zilizofungashiwa virago zianze tena maana elimu hii bado inahitajika sana - hiki si kitu cha siku moja.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa ipo haja kwa watoto wadogo kuanza kuelimishwa juu ya umuhimu wa kulipa kodi ili watoto wakue wakijua kwamba ukwepaji wa kodi ama upokeaji na utoaji wa rushwa ni jambo la aibu katika familia.

MWIGULUU%2011.jpg

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo ameitoa leo Juni 24, 2021, Bungeni Dodoma na kuongeza kuwa taifa litakalojengwa na watu wa aina hiyo litakuwa ni bora zaidi na kwamba jamii ya sasa haijafikia hatua ya watu kuonashida kujihusisha na masuala ya rushwa na na ukwepaji wa kodi.

"Tumeendelea kuongea na wenzetu wa Wizara ya Elimu kwamba tunakijenga vipi kizazi cha nchi yetu tangu wakiwa wadogo waelewe masuala ya wajibu, kodi na kupinga rushwa, watoto wetu tukiwaambia tangu wadogo wakaanza kuona ni aibu kukamatwa kwenye masuala ya kukwepa kodi, tangu wapo shuleni wakaanza kuona ukionekana unakwepa kodi ama rushwa ni jambo la aibu kwenye familia yenu Taifa litakalojengwa na kizazi cha aina hicho ni bora sana," amesema Dkt. Nchemba.
watu walipe kodi nyie wabunge mjilipe mamilioni na bado mnaona hayatoshi
 
Mh. Mwigulu unazungumzia kukwepa kulipa kodi kwa maana ya "tax evasion" ama "tax avoidance" ama vyote viwili? Nasema hivi kwa sababu viongozi wakuu wamejitengezea mazingira ya kisheria ya kutokulipa kodi na wala hawaoni aibu yoyote ile.

Hivi utamfundishaje mtoto wa mlalahoi ambaye mzazi wake anapata kipato kiduchu na kulazimika kulipa kodi, huku upande wa pili kuna viongozi wa juu wa nchi licha ya vipato vyao kuwa ni vikubwa na malupulupu kibao lakini hawapaswi kulipa kodi? Je watoto wetu wakiuliza, "Hivi viongozi wetu hawaoni aibu ya kutokulipa kodi?" Tutawapa majibu gani?
 
Back
Top Bottom