Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea Mwenza wa Urais 2025, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kufanya mkutano na wananchi wa Wilaya ya Namtumbo, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuimarisha sekta ya kilimo na kuahidi kushughulikia ujenzi wa soko na stendi ya kisasa katika mji huo.
Akizungumza Aprili 3, 2025, Dkt. Nchimbi amewashukuru wananchi kwa mapokezi ya kishindo na kuwapeleka salamu za upendo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akionesha kufurahishwa na uhai wa chama wilayani humo, akiipongeza CCM kwa kuendelea kujibu kero za wananchi.
Akizungumzia maendeleo ya kilimo, Dkt. Nchimbi amepongeza Wilaya ya Namtumbo kwa kushika nafasi ya pili kimkoa kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali na kuwa ya kwanza kwa uzalishaji wa tumbaku.
"Mnatoa heshima kubwa kwa Mkoa wa Ruvuma kwa uchapakazi wenu. Tuendelee kuchapa kazi tukijua kazi ni kipimo cha utu," alisema.
Ameeleza kuwa kwa miaka 10 mfululizo, Tanzania imekuwa ikijitosheleza kwa chakula, huku Ruvuma ikiwa miongoni mwa mikoa mitano bora kitaifa kwa uzalishaji wa chakula.
Sambamba na hilo, ametoa wito kwa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) na Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbegu bora zinapatikana kwa urahisi kwa wakulima kupitia wakala wa karibu. Aidha, ameitaka ASA kuongeza uzalishaji wa mbegu hizo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Vita Kawawa, amemshukuru Rais Samia kwa kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji wilayani humo.
Ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utaanza muda mfupi ujao. Pia alieleza mafanikio mengine katika sekta ya elimu ambapo madarasa 207 yamejengwa, pamoja na zaidi ya Shilingi Bilioni 6 kutumika katika sekta ya afya.
Hata hivyo, Mbunge huyo ameainisha changamoto kadhaa, ikiwemo upungufu wa watumishi wa umma na ubovu wa miundombinu ya barabara, akitaja barabara ya Mtwara Pachani-Lusewa-Tunduru na Lumecha-Hanga-Kitanda-Malinyi kupitia Ifakara, ambazo ameomba zijengwe kwa kiwango cha lami.