Dkt. Nchimbi adaiwa kuonekana Dubai, mapumzikoni. Je ni yeye au picha za AI?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
23,234
Reaction score
28,473


=====

Aliyekuwa Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameonekana nchini Dubai hivi karibuni akiwa kwenye mapumziko, taarifa ambazo zinafuta uvumi uliokuwa ukienea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kutoonekana kwake wiki kadhaa tangu ajiuzulu

Taarifa za vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa Dkt. Nchimbi yupo nchini humo kwa ajili ya shughuli zake binafsi; akiwa mzima na mwenye afya.

Wakati wa mizunguko hiyo, Dkt. Nchimbi alionekana akiwa ameambatana na mtu mmoja ambaye kwa muonekano wake anasadikiwa kuwa ni msaidizi wake.

Kuonekana kwa kiongozi huyo kunawapa majibu wananchi kufuta hofu na madai yaliyokuwepo kuwa ametekwa.

 
Hizi ni propaganda za kuhamisha upepo, na hizi ni habari za kupika...
Hizo picha ni full AI...

Hii picha, hayo ni meno? Ama ndevu? Kama ni meno hapa AI imeteleza...



Huo mkono haupo sahihi ulivyokaa na jinsi ulivyoshika simu...


Hiko kidole kimekatika ama kimeenda wapi? , na hata hiko kidole gumba AI imeteleza hapo.., hakuna kidole gumba kimekaa hivyo , Hii ni AI...



Hizi picha ni AI...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…