Dkt. Nchimbi ahimiza Watanzania tupambanie Katiba Mpya. Ni yeye au AI?

Anachoongea ni sahihi kiuzalendo, ila anakosa mikakati ya ushindi.

Kwa ccm ili wakuteue inatakiwa ufiche makucha kwanza, wasijue maoni na misimamo yako. Huyu wenzake watamuona hafai
 
Wasira tena?🤣🤣🤣🤣
Anatamani arudi tu kule hifadhi ya Gombe akajilie matunda pori yake
FB_IMG_1756217929952.jpg
 
Anachoongea ni sahihi kiuzalendo, ila anakosa mikakati ya ushindi.

Kwa ccm ili wakuteue inatakiwa ufiche makucha kwanza, wasijue maoni na misimamo yako. Huyu wenzake watamuona hafai
Hilo lipo kwani ndani ya ccm ukiwa mkweli basi utaonekana ni msaliti na mpinzani.

Ila wasijizime data kwa brother Nchimbi maana yeye anaijua vema ccm kuliko hao wahamiaji
 
Maana yake ni kuwa kama taifa tunatakiwa kuanza upya kujenga msingi wa nchi hii tukianzia pale alipokosea Mwalimu Julius Nyerere, Hakuitendea haki Tanganyika na ndio msingi wa mfarakano huu ambapo vyama vya siasa na hasa CCM vimejimilikisha mamlaka ya Dola.
Ili kufanikisha lengo tarajiwa ambalo ni ustawi wa haki na maendeleo ya nchi hii, ni lazima wananchi wote wa nchi hii washiriki kikamilifu kutoa mawazo juu ya Katiba ya wananchi, wote wanaoshikiriwa magerezani na waliopotezwa kwa lengo la kuendelea kuwa madaraka warudishiwe uhuru wao ili majadiliano yafanyike ya namna ya kuwajibishana au kushitakiana.
 
Hatuna sababu ya kumtilia mashaka. Kama ilivyo kwa mzee wetu Jaji Warioba, Dr. Nchimbi ni miongoni mwa makada wa CCM wanaojulikana kwa kusimamia wanachokiamini.

Mtakumbuka akiwa mjumbe wa kamati kuu, alitangaza hadharani kujitenga na uamuzi wa kamati kuu uliomuengua Mh. Lowasa kugombea urais.

Tofauti na wabunge wengi ambao wao kustaafu ni eirher ashindwe uchaguzi au afariki, Dr. Nchimbi, alitangaza kustaafu kugombea ubunge kwa hiari baada ya kuwa mbunge kwa vipindi viwili.

Akiwa katibu mkuu wa CCM, alipiga marufuku wimbo wa CCM unaosema, "Wapinzani, tuwalete, tuwachanechane, tuwatupe" Aidha ndie kiongozi pekee aliyemkemea, kada wetu wa UVCCM aliyewaambia polisi, "Tukiwapoteza wanaotukana viongozi msiwatafute"

Sina mashaka kuwa ni hii misimamo yake ndiyo iliyopelekea amebatizwa jina la YUDA.
 
Ni zao la october 29 au umelisahau hilo ?
 
Nimekubali maneno yako kiongozi,Wacha Sasa tusubirie reaction kutoka kwa wenye mamlaka zaidi yake
 
Hatuna sababu ya kumtilia mashaka. Kama ilivyo kwa mzee wetu Jaji Warioba, Dr. Nchimbi ni miongoni mwa makada wa CCM wanaojulikana kwa kusimamia wanachokiamini.

Mtakumbuka akiwa mjumbe wa kamati kuu, alitangaza hadharani kujitenga na uamuzi wa kamati kuu uliomuengua Mh. Lowasa kugombea urais.

Tofauti na wabunge wengi ambao wao kustaafu ni eirher ashindwe uchaguzi au afariki, Dr. Nchimbi, alitangaza kustaafu kugombea ubunge kwa hiari baada ya kuwa mbunge kwa vipindi viwili.

Akiwa katibu mkuu wa CCM, alipiga marufuku wimbo wa CCM unaosema, "Wapinzani, tuwalete, tuwachanechane, tuwatupe" Aidha ndie kiongozi pekee aliyemkemea, kada wetu wa UVCCM aliyewaambia polisi, "Tukiwapoteza wanaotukana viongozi msiwatafute"

Sina mashaka kuwa ni hii misimamo yake ndiyo iliyopelekea amebatizwa jina la YUDA.

Mkuu Dr Adam Francis, naona unalazimisha kutuaminisha usanii mchana kweupe, lakini hapa jukwaani haupo na mazuzu! Huyo Dr. Nchimbi unayemvika utakatifu leo, ndiye yuleyule mwanasiasa anayejua kucheza na akili za watu akitafuta maslahi yake ya baadae. Unasema ana msimamo? Msimamo gani wakati amekaa kimya akibariki uporaji wa haki za watanzania?
Ukweli unaoukwepa ni huu:
  • Mratibu Mkuu wa Sinema za Uchaguzi: Akiwa Katibu Mkuu wa CCM, yeye ndiye injini na mratibu mkuu wa dhihaka zote zilizofanyika kwenye chaguzi zilizopita. Huwezi kututenganishia Katibu Mkuu wa chama na ushuni uliotendeka uwanjani!
  • Ukimya wa Kinafiki Kwenye "Uchafu": Wakati wapinzani wakienguliwa kwa hila, mawakala wakipigwa na kufungiwa nje, na masanduku yakijazwa kura za mchongo, mbona huyo "mtu wa misimamo" hakunyanyua mdomo wake kukemea? Kama viongozi wa upinzani wanavyosema: "Ukikaa kimya wakati wa dhuluma, wewe ni mshiriki wa dhuluma hiyo." Alifurahia ushindi wa mezani, leo hii anataka pambio gani hapa?
  • Kiini Macho cha 2030 (Political Rebranding): Hizi kauli zake za sasa za kujifanya nabii wa Katiba Mpya ni ujanja wa kitoto wa kusafisha nyota yake (political rebranding) kuelekea mbio za urais wa 2030. Upinzani ulishamshtukia kitambo: "Hawawezi kuwa wale wale waliolinda na kufurahia mifumo ya ukandamizaji jana, leo wanapopoteza nguvu wajifanye manabii wa Katiba Mpya. Huu ni usanii!"
  • Mamluki wa Maslahi ya Makundi: Hiyo mifano ya nyuma unayomsifia nayo (kama ya Lowassa) haikuwa kwa ajili ya mtanzania wa kijijini, bali yalikuwa ni mapambano ya matumbo na ushawishi wa makundi ndani ya CCM yao.
  • Maneno Matamu, Vitendo vya Kidikteta: Kupiga marufuku wimbo wa "kuwakata vipande" wapinzani jukwaani is usanii wa kisiasa. Mbona nyuma ya pazia mfumo wake unaendelea kukandamiza demokrasia? Kama wanaharakati wanavyosema: "Tanzania haitaji viongozi wajanja wanaojua kusema maneno yanayofurahisha masikio ya wananchi huku mfumo wao ukiendelea kuumiza watu."
Acheni kutufanya watanzania wajinga. Tunafuatilia kila kitu na tunajua nani anatafuta kura za mbele. Hawezi kuwa mbunifu wa tatizo jana, alafu leo ajifanye ndio daktari wa tiba!
 
Ni zao la october 29 au umelisahau hilo ?
Mkuu Al Watani, umegonga ndipo na umeweka nukta pale palipostahili! Hakika umemrudisha Dr Adam Francis darasani mchana kweupe.
Umesema ukweli mchungu ambao makada wa CCM wanatamani watanzania waupotezee. Hiyo tarehe 29 October na hiyo dhihaka ya "amri kutoka mamlaka ya juu" ndiyo iliyozika kabisa demokrasia yetu, na Dr. Nchimbi akiwa Katibu Mkuu ndiye aliyekuwa msimamizi na mratibu mkuu wa mfumo huo.
Huwezi kuwa mbunifu au mshiriki wa ule "uchafu" wa jana, alafu leo kwa sababu tu unatafuta kura za mbele za 2030, uanze kujivika joho la utakatifu na kujifanya nabii wa Katiba Mpya au maridhiano. Sisi siyo mazuzu, tunajua kabisa huu ni usanii na mkakati wa kusafisha nyota yake (political rebranding). Hawezi kukwepa hiyo dhambi!
 
Back
Top Bottom