Dkt. Nchimbi Amuagiza Bashungwa, Ujenzi wa Barabara ya Kyerwa - Karagwe Kuanza

Dkt. Nchimbi Amuagiza Bashungwa, Ujenzi wa Barabara ya Kyerwa - Karagwe Kuanza

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

DKT. NCHIMBI AMUAGIZA BASHUNGWA, UJENZI WA BARABARA YA KYERWA - KARAGWE KUANZA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuelekeza Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kuhakikisha utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Kyerwa - Omurushaka Karagwe (km 62.5) kwa kiwango cha lami unaanza mara moja ili kuondoa adha wanazozipata wananchi wa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo leo tarehe 08 Agosti, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kyerwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stendi ya Mabasi ya Nkwenda, Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa lengo la ziara yake ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuimarisha Chama cha Mapinduzi.

“Huu ni Mkoa wa 15 tukiendelea kusikiliza kero za wananchi na kakagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na hapa changamoto yenu kubwa ni barabara ya kyerwa hadi Omurushaka”,amesema Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongzwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Kagera imepokea fedha kutoka Serikali Kuu jumla ya Shilingi Trilioni 12 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Miundombinu, Afya, Elimu na Umeme ili kuhakikisha maisha ya wana Kagera yanabadilika.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuahidi Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi kumleta na kumkabidhi kwa wananchi Mkandarasi aliyepatikana kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Kyerwa - Omurushaka (km 62.5) kwa kiwango cha lami.

Bashungwa ameeleza kuwa tayari Mkandarasi ameshaoneshwa eneo la kujenga Kambi na eneo la kuweka mitambo ili kuanza ujenzi wa barabara hiyo
 

Attachments

  • DKT. NCHIMBI AMUAGIZA BASHUNGWA UJENZI WA BARABARA YA KARAGWE - KYERWA KUANZA.mp4
    33.2 MB
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.56.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.56.jpeg
    284.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.57.jpeg
    569.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.57(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.57(1).jpeg
    228.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.57(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.57(2).jpeg
    276.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.58.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.58.jpeg
    764.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.58(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.58(2).jpeg
    613.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.59.jpeg
    738.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.59(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.59(1).jpeg
    790.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.59(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-08 at 15.05.59(2).jpeg
    258.3 KB · Views: 3
Hivi si ndiye huyu alikuwa anamsema Makonda kwa kutoa maagizo kwenye media????? Comrade Mungu amsaidie utambuzi
 
Back
Top Bottom