Dkt. Nchimbi amwakilisha Rais Samia Congo kwenye Mkutano wa wakuu wa Nchi-ICGLR

Dkt. Nchimbi amwakilisha Rais Samia Congo kwenye Mkutano wa wakuu wa Nchi-ICGLR

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Tisa wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), uliyofanyika, jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na vikao vya Wataalam, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi pamoja na Kamati za Mawaziri wa Kisekta, ikiwemo Ulinzi, Madini na Jinsia, umebebwa na kauli mbiu ya “Uimarishaji wa Amani na Usalama kwa Maendeleo Endelevu katika Eneo la Maziwa Makuu”

Kupitia kaulimbiu hiyo, nchi wanachama zimejadili hali ya usalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu na kupendekeza njia za kuimarisha amani na usalama kwenye eneo hilo.

Katika Mkutano huo, Tanzania inaunga mkono ajenda zote muhimu zilizojadiliwa ikiwemo ya amani na usalama na kusisitiza kuwa itaendelea kutoa mchango mkubwa kama inavyofanya katika nchi mbalimbali kuhakikisha kuwa amani ya kweli inapatikana kwenye Kanda hiyo.
 
Samuya anaishi kama digi digi😂😂
 
Huyo bwana atapiga sana misele awamu hii hata Mpango akasome!
 
Samuya anaishi kama digi digi😂😂
ndio ilikuwa dili zake hizi! sahivi ataenda Dubai tu kuzungushwaa na vitoroli mjini mule huku akipunga mkono ndani ya vigari kama vigari vya watoto mlimani city na China kuonyeshwa tu sehemu wanakoficha ela bas
 
Back
Top Bottom