Dkt. Nchimbi Awaagiza Mwigulu & Bashungwa Ulipaji Fidia Bukoba Mjini

Dkt. Nchimbi Awaagiza Mwigulu & Bashungwa Ulipaji Fidia Bukoba Mjini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

DKT. NCHIMBI AWAAGIZA MWIGULU NA BASHUNGWA ULIPAJI FIDIA BUKOBA MJINI.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amemuelekeza Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kuiwezesha Wizara ya Ujenzi kiasi cha Shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa upanuzi wa njia nne wa barabara ya Bukoba Mjini kuanzia Rwamishenye Roundabout hadi Stendi Mpya ya Bukoba Mjini (km 1.2) ambao utekelezaji wake unaendelea.

Dkt. Nchimbi ametoa maelekezo hayo Mkoani Kagera wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bukoba Mjini ambapo pamoja na mambo mengine amesikiliza na kutatua kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi.

“Nitumie nafasi hii kumtumia salamu Waziri wa Fedha huko huko alipo kwa uzito wake, Dkt. Mwigulu hawezi kushindwa kutafuta Bilioni 1.8 kwa muda mfupi, Kwahivyo naielekeza Wizara ya Fedha kutafuta hizi fedha haraka sana kwa ajili ya fidia za wananchi wa Bukoba Mjini”, amesisitiza Dkt. Nchimbi.

Awali, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inaendelea na upanuzi wa barabara njia nne kuanzia Rwamishenye Roundabout hadi Stendi Mpya ya Bukoba Mjini ambapo ujenzi huo ukikamilika itaendelea na Awamu ya Pili kuanzia Rwamishenye hadi Stendi Mpya ya Kyakailabwa na Awamu ya Tatu kuanzia Stendi ya Mpya ya Bukoba Mjini hadi Bandari ya Bukoba (Customs).

Aidha, Bashungwa amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mingi ya kimkakati katika Sekta mbalimbali na hata ile ambayo ipo katika mpango wa kuanza kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Ndege cha Omukajunguti Mkoani Kagera.

Kwa upande, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Stephen Byabato ameeleza kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 16 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara inayoendelea kutekelezwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) katika jimbo la Bukoba Mjini.
 

Attachments

  • DKT. NCHIMBI AWAAGIZA MWIGULU NA BASHUNGWA ULIPAJI FIDIA BUKOBA MJINI...mp4
    34.7 MB
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.37.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.37.jpeg
    279.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.38.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.38.jpeg
    263.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.38(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.38(1).jpeg
    592.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.39.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.39.jpeg
    295.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.39(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.39(1).jpeg
    787.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.40.jpeg
    584.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.41.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.41.jpeg
    482.5 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.41(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.41(1).jpeg
    823 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.42.jpeg
    420.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.42(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-11 at 13.11.42(1).jpeg
    794.7 KB · Views: 7
Back
Top Bottom