Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: CCM ikitikisika hakuna Tanzania madhubuti

Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: CCM ikitikisika hakuna Tanzania madhubuti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ripoti ya CAG imewahi taja Majina specific ya wezi? Huwa unafuatilia masuala ya Serikali na mahakama?
Kwahio wenye office husika ni mazombi wasioonekana!!?

Kama office Ina hati chafu mwenye office ndio kafanikisha uchafu wa hati hiyo au we unaonaje!!!

Mnataka ataje wakati office zinajulikana!!?

Mwanasheria mkuu alipaswa kuwashtaki wenye office husika!
 
Wananchi hatuitaki CCM isiojali maslahi ya umma na badala yake kujifanyia ujambazi wa rasilimali na kulindana kwa vyeo na kupuuza katiba ya nchi. Watu wanaiba mambilioni wamekaliwa kimya tu. Mwananchi akipitisha kodi ya mwezi wala hacheleweshwi ni mvua chap mafaini kibao na kufungiwa biashara watatumwa maofisa kama ishirini.

Hio sio CCM aliyoiasisi Mwalimu Nyerere na tunatamani ichanike chanike hata jioni ya leo. Yani hali ilipofikia ukiweka picha ya mbuzi na Mgombea wa CCM watu wanaweza kumpa kura mbuzi 😁
 
Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi amesema maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere bado yanaishi ya kwamba CCM ikitikisika hakutokuwa na Nchi madhubuti na hivyo amewataka kila Mtanzania moyoni mwake asikie kwamba uimara na umadhubuti wa Nchi unamtegeme.

Akiongea Mkoani Singida leo May 30,2024, Nchimbi amesema “Maneno ya Baba wa Taifa bado yanaishi, CCM ikitikisika hatuna Nchi madhubuti, kila mmoja wenu moyoni mwake asikie kwamba uimara na umadhubuti wa Nchi yetu unamtegemea”

“Kila Mtu akijisikia hivyo kila Mtu atatimiza wajibu wake, tuwapende Watu kwa dhati na Watanzania wajue Viongozi wa CCM wanawapenda na wapo tayari kuwatumikia, Watanzania wakijua hivyo wataendelea kuichagua CCM"

My Take
Naunga mkono hoja ya Dr.Nchimbi kwani tumeona Vurugu, ngumu na Rushwa zilivyorindima kwenye chaguzi za Vyama maslahi kiasi kwamba unajiuliza Hawa wakipewa Nchi itakuaje?

Hakuna Taifa bila CCM. Kazi iendelee.

View: https://www.instagram.com/p/C7lbT2LKGuX/?igsh=MTJpNmxkcDc5N3Zsdg==

Majitu yamelewa uongo wao wenyewe mpaka wanaamini ni ukweli
 
kwa hiyo Bw. Nchimbi sisi wananchi tuvumile jini CCm akiendelea kutukausha damu?? huu uongo kama wa yule jamaa aliyetuambia 'Saddam hussein rais wa Kuwait'.
Wananchi wanahitaji mabadiliko hakuna litakalowarudisha nyuma.
 
CCM imara iliondoka na Nyerere! CCM iliyopo ni legelege sema inabebwa na kushikiliwa na
 
Walioishiwa hoja ni CCM au Wapinzani wanaoongea ubaguzi?

Pili maendeleo unayoyaona Leo kimeleta chama gani? 😆😆😆

Au kwako maendeleo ni tofauti na hiki hapa 👇

View: https://www.instagram.com/p/C7nvXn-CCD_/?igsh=MXdiOXRwaGV4bzg3OA==

Maendeleo gani unayoona ccm imeleta? Kwanza ushahidi wa kuwa chama hicho kimeshafilisika ni hiyo habari hapo ya kutaja serikali ya fulani na ya awamu fulani. Ukiona hivyo ujue walishajua wananchi wamewakataa ndio maana huoni ikitajwa serikali ya watanzania kwa sababu hata wao wanajua watanzania katika wingi wao hawakuichagua ccm.
 
Kiufupi Chadema sio tuu wajinga Bali ni wapuuzi ndio maana mnahubiri ubaguzi
Wewe nawe uache kupayuka. Nchimbi kaongelea CCM wewe unawaza CHADEMA. CHADEMA wametumia wanafanya chaguzi zao. Nyie endeleeni kubwabwaja.
 
Wewe nawe uache kupayuka. Nchimbi kaongelea CCM wewe unawaza CHADEMA. CHADEMA wametumia wanafanya chaguzi zao. Nyie endeleeni kubwabwaja.
Bwaaaa bwaaaaa ila Chadema ni looser na hopeless
 
Back
Top Bottom