GE2025 Dkt. Nchimbi: CCM kugharamia matibabu ya saratani na figo ndani ya siku 100 za kwanza madarakani

GE2025 Dkt. Nchimbi: CCM kugharamia matibabu ya saratani na figo ndani ya siku 100 za kwanza madarakani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Waongo wazushi tu

Nishauguza mgonjwa alikuwa na pancreatic cancer mbilinge na gharama tulizopitia tunazijuwa

Hawa wanasiasa waache uhuni wa kucheza na akili za wajinga

Kwanini wasubirie mpaka uchaguzi uishe ndy watoe huo unafuu wanaosema

Huo ni uwongo uwongo tu

Ova
Hapo na kuna watu watafurahia. Labda hizo huduma bure ni kwa ma kada
 
Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewakumbusha Watanzania kuhusu ahadi za Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizoziahidi kutekeleza ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena nchi.

Amesema hayo alipowasili katika Kata ya Mkula, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, leo Septemba 1, 2025, kwa ajili ya kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025–2030.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa, ndani ya siku 100 za kwanza Madarakani, Serikali ya CCM itaanza kugharamia matibabu ya magonjwa yanayowatesa Watanzania, ikiwemo saratani na magonjwa ya figo.

Tuambiwe ndani ya siku 100 Bunge litapitisha bajeti mpya vinginevyo ni uchuro! Kwa nini matibabu hayo yasianze sasa kama ni kwa kutumia bajeti hii hii ya 2025/26!
 
Back
Top Bottom