mrxtz2026
JF-Expert Member
- Jan 24, 2026
- 609
- 1,314
Katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametoa kauli nzito kuhusu Katiba Mpya. Alisema ikiwa angepewa nafasi ya kutoa ujumbe mmoja wa mwisho kwa Watanzania, ujumbe huo ungekuwa mmoja tu:
"Kama nina kitu cha kuwaambia Watanzania, ningewaambia pambaneni mpate Katiba Mpya itakayodumu miaka 50, yenye mwafaka katika Taifa, itakayotupeleka mbele miaka 50."
Aliongeza kuwa lengo la Katiba Mpya halipaswi kuwa kushinda au kushindwa kwa upande mmoja, bali kujenga msingi wa umoja, utulivu, haki na maendeleo endelevu ya Taifa. Alieleza kuwa Katiba imara hujengwa kwa maridhiano mapana yanayowakutanisha Watanzania wenye mitazamo tofauti, wakiweka mbele maslahi ya Taifa badala ya maslahi binafsi au ya kisiasa.
Kwangu, maneno haya yanaibua jambo la msingi ambalo Watanzania wengi hawalifahamu. Katiba ni sheria kuu ya nchi, na kwa mujibu wa Ibara ya 64(5) ya Katiba ya mwaka 1977, sheria yoyote inayokinzana na Katiba ni batili kwa kadri ya mkinzano huo. Kwa mantiki hiyo, hakuna sheria ya kawaida inayoweza kuisimamisha Katiba; ni Katiba inayozipima sheria zote. Hii ndiyo maana ubora wa Kataba yenyewe ni suala la uhai wa Taifa.
Wito wa Makamu wa Rais wa kupambania Katiba ya mwafaka unagusa hoja moja ya kifalsafa ambayo ni muhimu kuiweka wazi. Katika nadharia ya kikatiba, mamlaka ya kutunga Katiba (pouvoir constituant) ni ya wananchi wenyewe, siyo ya viongozi. Ndiyo maana wito huo haumaanishi kupambana na mtu, bali kutimiza wajibu wa kiraia wa kushiriki katika kuunda msingi wa Taifa. Swali la msingi si "tunapambana na nani", bali "je, tumejiandaaje kutumia mamlaka haya tuliyonayo kama wananchi".
Ni katika muktadha huu ninapenda kuelekeza macho ya kitaaluma, kisomi na kiraia kwenye rasimu kamili ya pendekezo la Katiba iliyopo www.katibampya.com. Rasimu hii ina mambo mawili yanayostahili uchunguzi wa karibu.
Kwanza, Ibara ya 176 na Sura ya Pili zinaanzisha utaratibu wa kuhakiki uhalali wa uongozi kabla ya kuapishwa, jambo linaloimarisha uadilifu wa mchakato wa madaraka.
Pili, na hili ndilo kubwa zaidi, rasimu inapendekeza muundo wa Mihimili Minne, siyo mitatu. Mbali na Bunge, Mahakama na Serikali, kunaongezwa Baraza la Usimamizi wa Taifa kama muhimili wa nne ulio sawa kikatiba na mihimili mingine. Muundo huu unalenga kuziba mianya ya usimamizi ambayo katiba nyingi hushindwa kuiziba.
Makamu wa Rais ameomba mwafaka na uchunguzi wa wazi. Rasimu hii ipo tayari kwa uchunguzi huo. Nawaalika wanazuoni, wanasheria, asasi za kiraia na kila Mtanzania anayeijali nchi yake kuisoma, kuihoji na kuichambua.
Tukutane www.katibampya.com