Dkt. Ndubaro amuongezea faini babu wa TikTok

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Your browser is not able to display this video.

Seif Kisauji 'Babu wa TikTok'
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro ameongeza adhabu ya faini kutoka shilingi milioni 3 hadi milioni 5 msanii Seif Kisauji maarufu 'Babu wa TikTok' akimtaka msanii huyo aombe msamaha hadharani kutokana na kosa la kurusha maudhui ya sanaa yanayokiuka maadili mtandaoni.

Waziri Ndumbaro ametoa uamuzi huo leo Jijini Dodoma baada ya kusikiliza rufaa ya msanii huyo ya kupinga adhabu aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa kwa miezi sita pamoja na kulipa faini ya TZS milioni 3 kutokana na kurusha mtandaoni picha za video zinazokiuka maadili.

Aidha, kufuatia rufaa hiyo, msanii Seif Kisauji amekiri kosa la kusambaza maudhui hayo na kuomba apunguziwe adhabu, hatua iliyomfanya Waziri Dkt. Ndumbaro amuondolee adhabu ya kifungo cha cha miezi 6 cha kutojihusisha na shughuli za sanaa huku akimuongezea kiwango cha faini kutoka milioni 3 hadi 5.

PIA SOMA
- Kisauji (babu wa TikTok) afungiwa miezi sita
 

Attachments

  • Screenshot_20240903-171118_1.jpg
    109.8 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…