Dkt. Ndugulile ataka ushiriki wa Sekta Binafsi katika kuelekea uchumi wa kidijitali

Dkt. Ndugulile ataka ushiriki wa Sekta Binafsi katika kuelekea uchumi wa kidijitali

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
NDUGULILE ATAKA USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KATIKA KUELEKEA UCHUMI WA KIDIJITALI

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile (Mb) ameitaka sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuleta mapinduzi ya TEHAMA kwa lengo la kuelekea uchumi wa kidijitali.

Dkt Ndugulile aliyasema hayo aliposhiriki kwenye mkutano kupitiq mtandao (Zoom meeting) na watendaji wakuu wa makampuni binafsi kupitia umoja wao (CEOrt).

Dkt Ndugulile aliwaeleza kuwa Serikali inaendelea kuwekeza kwenye mazingira wezeshi ya kukuza sekta ya TEHAMA na katika kuelekea uchumi wa kidijitali. Dkt Ndugulile ameitaka Sekta binafsi kusaidiana na Serikali katika kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani, kuwekeza kwenye viwanda vya vifaa vya TEHAMA na kusambaza mawasiliano katika maeneo ya pembezoni.

CEOrt kupitia kwa Mwenyekiti wao Bw Sanjay Rughani wameahidi kushirikiana na Serikali katika kuleta mapinduzi makubwa ya TEHAMA hapa nchini na wameahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali pale watakapohitajika.

Mkutano huo umeudhuriwa na Watendaji Wakuu wa Makampuni binafsi wapatao 50.

IMG-20210504-WA0098.jpg


IMG-20210504-WA0099.jpg
 
Isije ikawa kama mambo ya bando tu
 
1. Paypal , skrill na online wallet zisiwafanye kizazi cha sasa kutumia nguvu kubwa kuzitafuta✅

2. Online transaction zisiwe na vikwazo vingi✅

3.Biashara za online kama bitcoin kama mataifa mengi duniani yanakubali sisi ni nani tubaki nyuma?✅
 
Back
Top Bottom