Aliyewahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Internet ni nyenzo muhimu kwenye kuchochea maendeleo.
Kupitia andiko lake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Dkt. Ndungulile amesisitiza umuhimu huduma hii kupatikana kirahisi, kwa gharama rafiki ikiwa na ubora wa hali ya juu.
Aidha, Serikali, Asasi za kiraia, Makampuni binafsi pamoja na wanazuoni ni washirika muhimu kwenye kuchochea maendeleo ya sekta hii muhimu ya mawasiliano.
Dkt. Ndungulile aliwahi pia kuhudumu kama Naibu Waziri wa Afya kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Hayati John Pombe Magufuli Mei 16, 2020.
Huyu Dr. Ndungulile hapaswi kusikilizwa kwa chochote kwa sasa kuhusu hili, maana upuuzi wote wa makato, tozo na kubaniwa mabundle ya data ulianzia wakati yeye akiwa ni waziri husika.