Dkt. Ndugulile: Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi inakuja

Dkt. Ndugulile: Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi inakuja

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1643804099421.png

Picha: Dkt Faustine Ndungulile

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndungulile ameeleza azma ya serikali katika kuanzisha Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi (Personal Data Protection). Dkt. Ndugulile amesema serikali inathamini jambo hili linalozidi kuwa maarufu ulimwenguni ambalo linachochewa na ukweli kwamba kwa sasa shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi zinafanyika mtandaoni.

Wakati katiba inahakikishia haki ya faragha na sheria zingine zinathamini umuhimu wa utunzaji wa taarifa binafsi, Tanzania haina sheria kamili inayoshughulikia maswala ya faragha na utunzaji wa data, mambo mawili ambayo yanazidi kuwa muhimu ikizingatiwa jinsi mitandao unavyoathiri maisha ya watu katika kila nyanja. Mazungumzo ya Tanzania kuja na muswada wa sheria ya faragha na ulinzi wa taarifa binafsi yamekuwa yakiendelea tangu 2018 lakini bila kuzaa matunda.

Akizungumza leo, Ijumaa, Julai 2, 2021, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Muhtasari wa Mfumo wa Dijitali, Teknolojia zinazoibuka na zinazotumiwa na NGOs nchini Tanzania na uhuishaji wa media tofauti kwenda mfumo wa kidigitali, iliyoandaliwa na kampuni ya Media Convergency, Dr Ndungulile alielezea wasiwasi wake kuhusu jinsi sheria ya Tanzania ambapo mfumo hauwezi kulinda habari za kibinafsi za watu, na kutaja mabadiliko ya hili kama moja ya vipaumbele vyake.

"Tunataka kuwapa watu wanaoingiliana na ulimwengu wa kidijitali udhibiti habari ambazo zinakusanywa kutoka kwao," alisema waziri huyo kijana na mjuzi wa mambo ya kidigitali. "Tunataka kuwafanya watu wafahamu ni data gani wanazozishea, ni kwa nani na zitatumiwaje."

Zaidi soma:
Communication and Information Technologies minister Dr Faustine Ndungulile reiterated the government’s intention to introduce the Privacy and Data Protection legislation in Tanzania yesterday, giving an impression of the government’s appreciation of the increasingly popular worldwide phenomenon which is motivated by the fact that more and more social and economic activities are taking place online.

While the constitution guarantees the right to privacy and other pieces of legislation appreciate the importance of data protection, Tanzania does not have a comprehensive law that addresses issues of privacy and data protection, two things which are increasingly becoming necessities given how digitization influences every aspect of people’s lives. Talks of Tanzania coming up with a bill on privacy and data protection law have been going on since 2018 but with zero results.

Speaking today, Friday, July 2, 2021, during the launching of a report An Overview of the Digital Ecosystem, Emerging and Applied Technologies on NGOs in Tanzania by Media Convergence, a local digital consultancy firm, Dr Ndungulile expressed his concerns at how Tanzania’s legal framework falls short of protecting people’s personal information, naming the changing of the status quo of one his ministries top priorities.

“We seek to give people interacting with the digital world to be in control of the information that is collected from them,” said the youthful and digital savvy minister. “We want to make people conscious of what data they share, to whom and how they are going to be used.”

Demonstrating how acute the situation is when it comes to data protection in Tanzania, Dr Ndungulile gave an example of a small study his ministry carried out in the Kinondoni district, Dar es Salaam which involved envelopes that pharmacists use when they give their customers the medicine they bought.

During the course of the study, the ministry’s team collected a total of 300 envelopes where 260 of them were found containing personal information. The personal information include medical reports; job application letters; passport applications; information about hotel bills, with the records of the nights spent there, who the companion was, what they ate and what they drank.

“So you can see how much information is out there,” Dr Ndungulile told the participants who had attended the occasion, which included Tanzania’s leading technology and digital stakeholders. “So we are going to come up with a law that addresses that.”

Ndungulile assured followers of Tanzania’s digital development that the preparation of the privacy and data protection law is in the final stages, assuring Tanzanians that the law’s aim is not to muzzle free speech but to protect users of various digital services available in Tanzania.

Source: The Chanzo Initiative
 
Tafsiri isiyo rasmi kwa hadhira ya kiswahili (Informal Transilation for swahili audience)

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndungulile alisisitiza azma ya serikali ya kuanzisha sheria ya Faragha na Ulinzi wa Takwimu nchini Tanzania jana, na kutoa taswira kwamba serikali inathamini jambo hili linalozidi kuwa maarufu ulimwenguni ambalo linachochewa na ukweli kwamba zaidi na zaidi shughuli za kijamii na kiuchumi zinafanyika mtandaoni.

Wakati katiba inahakikishia haki ya faragha na sheria zingine zinathamini umuhimu wa utunzaji wa data, Tanzania haina sheria kamili inayoshughulikia maswala ya faragha na utunzaji wa data, mambo mawili ambayo yanazidi kuwa muhimu ikizingatiwa jinsi mitandao unavyoathiri maisha ya watu katika kila nyanja. Mazungumzo ya Tanzania kuja na muswada wa sheria ya faragha na ulinzi wa data yamekuwa yakiendelea tangu 2018 lakini bila matokeo.

Akizungumza leo, Ijumaa, Julai 2, 2021, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Muhtasari wa Mfumo wa Dijitali, Teknolojia zinazoibuka na zinazotumiwa na NGOs nchini Tanzania na uhuishaji wa media tofauti kwenda mfumo wa kidigitali, iliyoandaliwa na kampuni ya ushauri wa kidijitali, Dr Ndungulile alielezea wasiwasi wake kuhusu jinsi sheria ya Tanzania ambapo mfumo hauwezi kulinda habari za kibinafsi za watu, na kutaja mabadiliko ya hili kama moja ya vipaumbele vyake.

"Tunataka kuwapa watu wanaoingiliana na ulimwengu wa kidijitali udhibiti habari ambazo zinakusanywa kutoka kwao," alisema waziri huyo kijana na mjuzi wa mambo ya kidigitali. "Tunataka kuwafanya watu wafahamu ni data gani wanazozishea, ni kwa nani na zitatumiwaje."

Kuonyesha jinsi hali ilivyo mbaya linapokuja suala la ulinzi wa data nchini Tanzania, Dk Ndungulile alitoa mfano wa utafiti mdogo wa wizara yake uliofanywa katika wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam ambao ulihusisha bahasha ambazo wafamasia hutumia wanapowapa wateja wao dawa walizonunua.

Wakati wa utafiti huo, timu ya wizara hiyo ilikusanya jumla ya bahasha 300 ambapo 260 kati ya hizo zilipatikana na habari binafsi. Habari binafsi ni pamoja na ripoti za matibabu; barua za maombi ya kazi; maombi ya pasipoti; habari juu ya bili za hoteli, na rekodi za siku uliokaa hapo, ulikuwa na nani, mlikula nini na mlikunywa nini.

"Kwahivyo unaweza kuona ni habari ngapi ziko nje," Dk Ndungulile aliwaambia washiriki ambao walikuwa wamehudhuria hafla hiyo, ambayo ilijumuisha wadau wa teknolojia Tanzania na wadau wa kidigitali. "Kwa hivyo tutakuja na sheria inayoshughulikia hilo."

Ndungulile aliwahakikishia wafuasi wa maendeleo ya kidigitali Tanzania kuwa maandalizi ya sheria ya faragha na ulinzi wa data iko katika hatua za mwisho, akiwahakikishia watanzania kuwa lengo la sheria sio kufunga midomo wa uhuru kusema bali ni kulinda watumiaji wa huduma za kidijitali zinazopatikana nchini Tanzania.
 
Huyu waziri anabwabaja sana wakati hakuna anachokijua kwenye issue za tech, ni aibu kuwa na waziri wa aina Hui

Subiria sasa hiyo sheria ya kulinda taarifa ije uone itakavyokuwa na double standard, NIDA ndio watu wa kwanza kabisa kuviolate haki ya faragha kwa hapa TZ
 
Huyu waziri anabwabaja sana wakati hakuna anachokijua kwenye issue za tech,ni aibu kuwa na waziri wa aina Hui

Subiria sasa hiyo sheria ya kulinda taarifa ije uone itakavyokuwa na double standard,NIDA ndio watu wa kwanza kabisa kuviolate haki ya faragha kwa hapa TZ
Tanzakiza
 
Back
Top Bottom