Dkt. Ndumbaro awataka waandishi kuepuka kuwa sehemu ya Ukatili wa kijinsia

Dkt. Ndumbaro awataka waandishi kuepuka kuwa sehemu ya Ukatili wa kijinsia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewaasa Waandishi wa habari kutotumia taaluma zao katika kusambaza taarifa ambazo zinachochea ukatili wa kijinsia bali wasimamie misingi ya uandishi na utoaji wa taarifa wenye lengo la kuelimisha na kuhabarisha na hatimaye kukuza ustawi wa jamii.

Waziri Ndumbaro ameyasema hayo tarehe 14/07/2023 wakati akizindua mafunzo ya siku mbili kwa Wahariri na Waandishi wa Vyombo vya Habari mbalimbali ambao wapo kwenye timu ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia inayosimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria.

“Ndugu zangu Wanahabari, wakati wa kuripoti masuala ya ukatili wa kijinsia, kumbukeni mnafanya kazi hii kwa lengo la kutokomeza masuala haya, naomba niwasihi msimamie misingi ya uandishi na utoaji wa taarifa kwa umma ili isije kuwa taarifa zenu badala ya kuonesha ubaya ili kuzuia uendelezwaji wa matukio haya, zikachochea tena ukatili”. Alisema Ndumbaro.

Aidha Ndumbaro aliwataka Wanahabari hao kujikita kwenye kutoa taarifa zenye mwendelezo wa ushughulikiwaji wa tukio husika kwa lengo la kusaidia wananchi kufahamu hatua zinazochukuliwa hadi kufikia haki ya muhusika.

Ndumbaro pia akavitaja vyombo mbalimbali vinavyotumika kumsaidia manusura ikiwemo huduma za usaidizi wa kisheria, simu za dharura, malazi na vituo vya dharura vya hifadhi ya manusura wa ukatili wa kijinsia huku akiwataka Wandishi kuzipa umuhimu taarifa hizi katika kurasa za kwanza za machapisho ili kusaidia kujenga ufahamu na uelewa kwa wananchi kuhusu wapi pa kukimbilia kupata msaada kunapotokea changamoto za ukatili wa kijinsia.

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi kutoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi alisema Wizara imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha mwananchi anapata huduma za kisheria kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

"Moja ya wadau tunaofanya kazi nao kwa ukaribu ni tasnia ya Habari kwa kuwa wana mchango mkubwa sana katika kuwafikia wananchi kupitia vipindi vya redio, televisheni na hata njia nyingine wanazozitumia" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria.

WhatsApp-Image-2023-07-14-at-10.16.50-PM-860x452.jpeg
WhatsApp-Image-2023-07-14-at-10.16.49-PM.jpeg
WhatsApp-Image-2023-07-14-at-10.36.51-PM.jpeg
WhatsApp-Image-2023-07-14-at-10.29.59-PM.jpeg
WhatsApp-Image-2023-07-14-at-10.17.02-PM.jpeg
 
Back
Top Bottom