Dkt. Ndyanao Balisidia aliyeimbiwa mwimbo wa harusi na kaka yake Patrick Balisidia miaka ya 70

View attachment 2140540

Mwanamuziki wa zamani Patrick Balisidia alizaliwa mwaka 1946, mwaka uliofuata yaani 1947 alizaliwa dada yake aliyepewa jina la Ndyanao.

Patrick na Ndyanao walielewana sana na walikua kama mapacha. Siku ya harusi ya Ndyanao, kaka yake Patrick alimuimbia mwimbo wa harusi ambao wengi mnaufahamu kama kuolewa’ ni jambo la sifa’.

Katika baadhi ya maneno ya mwimbo huu, yalisikika ‘ Ndyanao saiba’ huyu ndiye Ndyanano. Licha ya kuwa mkufunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr Ndyanao ndiye mtunzi wa kitabu cha Shida. Wengi miliki tumia kuji bia mtihani wa Kiswahili kidato cha nne.

Dr Ndyanao Balisidia ni miongoni mwa Tunu za Taifa letu, mama pumzika kwa amani.

Ni Moja wa co founder wa Band ya Afro 70, mwaka 1975 walipata accident mbaya sana na vyombo vyao vikaharibika vyote, toka hapo hawakuweza kusimama tena kama Band, akawa kama sole artist.

Alizaliwa Kongwa akasoma sekondari ya Dodoma na baadaye akachaguliwa kwenda DIT baada ya kuliza masomo ya chuo aliendelea maziki baadaye alienda kufanya mziki wake huko Sweden nadhani ndipo mauti ilimkuta.

Alifarika Mwaka 2004.
 
Yah Mkuu alivuta kitambo sana sema Fasihi andishi inamfanya aonekane yuko hai
Nadhani pia uchache wa vyombo vya habari na uduni wa mawasiliano vilichangia. Mwaka wa 1987 nilikuwa nimeshamaliza form four, na hicho kitabu nilikisoma na kukifanyia mtihani. Ndicho kitabu cha kiswahili nilichosoma na kukirudia mara nyingi kuliko vyote.
 
Hivi ule wimbo wa "🎶Ni mashaka ya maisha, wema hawana maisha 🎼" aliuimba mwaka gani? Ni baada au kabla ya kifo cha dada yake?

Nahisi aliudedicate kwa dada'ake maana ni kama dada alikuwa msaada mkubwa sana kwake.Ni wimbo ambao huwa unanitafakarisha sana.
 
View attachment 2140540

Mwanamuziki wa zamani Patrick Balisidia alizaliwa mwaka 1946, mwaka uliofuata yaani 1947 alizaliwa dada yake aliyepewa jina la Ndyanao.

Patrick na Ndyanao walielewana sana na walikua kama mapacha. Siku ya harusi ya Ndyanao, kaka yake Patrick alimuimbia mwimbo wa harusi ambao wengi mnaufahamu kama kuolewa’ ni jambo la sifa’.

Katika baadhi ya maneno ya mwimbo huu, yalisikika ‘ Ndyanao saiba’ huyu ndiye Ndyanano. Licha ya kuwa mkufunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr Ndyanao ndiye mtunzi wa kitabu cha Shida. Wengi miliki tumia kuji bia mtihani wa Kiswahili kidato cha nne.

Dr Ndyanao Balisidia ni miongoni mwa Tunu za Taifa letu, mama pumzika kwa amani.

Nzuri sana
Sikuijua hii
 
Hivi Nani alikua mtunzi wa kitabu Cha SIMU YA KIFO Cha akina mzee Jocob, FAMBO, Marry, Kefa, Agnes, Inspeta nani sijui,....kitabu kilivuta hisia sana kile.
 
Ila patrick balisidya aliurekebisha wimbo ulioimbwa na frank hamphling wa 1950s unaoitwa nyumbani ameingia tausi
Bwana mkubwa na wewe unamfaham Frenk Hamphling?basi utakua ni mfatiliaji wa mziki Sana huyu jamaa alikuaga na dadake wanaimba pamoja na walikua wenyeji wa Moshi lakini ni machotala nazani baba alikua mzungu na mama Yao ni mchaga.Watu wengi hawawafaham Mana wamevuma kabla Tanganyika haijapata uhuru .
 
Ni Moja wa co founder wa Band ya Afro 70, mwaka 1975 walipata accident mbaya sana na vyombo vyao vikaharibika vyote, toka hapo hawakuweza kusimama tena kama Band, akawa kama sole artist.

Alizaliwa Kongwa akasoma sekondari ya Dodoma na baadaye akachaguliwa kwenda DIT baada ya kuliza masomo ya chuo aliendelea maziki baadaye alienda kufanya mziki wake huko Sweden nadhani ndipo mauti ilimkuta.

Alifarika Mwaka 2004.
Chama Cha CCM kiliwazulimu Hawa jamaa Mana walipata ajali wakitoka kwenye shughuli ya chama na ilitakiwa walipwe kwa mujibu wa makubaliano lakini Toka enzi za Mkapa hawakulipwa hadi Leo.CCM lipeni fidia za watu kwa Sababu chanzo Cha kifo Cha Patrick Balisidya ni msongo wa mawazo kutokana na mkichomfanyiaga.
 
Hivi Nani alikua mtunzi wa kitabu Cha SIMU YA KIFO Cha akina mzee Jocob, FAMBO, Marry, Kefa, Agnes, Inspeta nani sijui,....kitabu kilivuta hisia sana kile.
Mwandishi wa kitabu cha simu ya kifo anaitwa Faraji Katalambula.
Nilikisoma kwa mara ya kwanza 1994.Fambo ni kifupisho cha Francis Andrew Mbozia,mtu aliyekua anabuni mauaji ya familia ya mzee Jacob,muuaji akiwa Agnes.
Mpelelezi alikua anaitwa inspekta Ringo.
 
Chama Cha CCM kiliwazulimu Hawa jamaa Mana walipata ajali wakitoka kwenye shughuli ya chama na ilitakiwa walipwe kwa mujibu wa makubaliano lakini Toka enzi za Mkapa hawakulipwa hadi Leo.CCM lipeni fidia za watu kwa Sababu chanzo Cha kifo Cha Patrick Balisidya ni msongo wa mawazo kutokana na mkichomfanyiaga.
Nyerere alitoa ahadi ya kuwapa vifaa na wakapata ,wakaenda navyo Nigeria (kama sikosei)kwenye tamasha la muziki walivyorudi wakanyang'anywa.
 
Ni Moja wa co founder wa Band ya Afro 70, mwaka 1975 walipata accident mbaya sana na vyombo vyao vikaharibika vyote, toka hapo hawakuweza kusimama tena kama Band, akawa kama sole artist.

Alizaliwa Kongwa akasoma sekondari ya Dodoma na baadaye akachaguliwa kwenda DIT baada ya kuliza masomo ya chuo aliendelea maziki baadaye alienda kufanya mziki wake huko Sweden nadhani ndipo mauti ilimkuta.

Alifarika Mwaka 2004.
Kazikwa makaburi ya buguruni malapa
 
Kiswahili ni kigumu kweli. Wakufunzi ndio watunzi wenyewe. Halafu wewe unasema "licha ya..." kana kwamba siyo kawaida kwa mkufunzi kutunga kitabu!!
Licha ya kuwa mkufunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr Ndyanao ndiye mtunzi wa kitabu cha Shida.
 
Back
Top Bottom