Pre GE2025 Dkt. Nshala alitishiwa maisha sababu ya kupinga Mkataba wa DP World. Uteuzi wake CHADEMA unamaanisha nini kwenye Siasa za Tanzania?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwamba unahisi ndo anaweza kuwa mgombea urais wa Chadema au umeona nini mkuu!!
Mgombea Urais sidhani, ila ataongeza nguvu kwenye kuiimarisha CHADEMA kuwa bora na yenye nguvu
 
Wakuu,

Januari 21 ulifanyika Uchaguzi Mkuu CHADEMA kwenye nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti kwa Bara na Zanzibar, ambako Lissu alitangazwa kuwa Mwenyekiti mpya CHADEMA, siku hiyo pia ulifanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama na Lissu akafanya uteuzi wa viongozi, na kati ya waliochaguliwa na Mwanasheria wa CHADEMA, Mjumbe wa Kamati Kuu Dkt. Nshala Rugemeleza.

Kwa wale waliokuwa wanafuatilia sakata la DP World jina hili la Nshala Rugemeleza sio jina geni kabisa. Umaarufu wake ulikua zaidi Juni mwaka 2023 alipojitokeza hadharani kupinga mkataba wa DP World kati ya serikali ya Tanzania na Dubai, mkataba ambao aliuita ni “batili” “kiuhaini” na “haramu”.

Nshala hakuishia hapo kwani alitangaza hadharani kuwa yupo mbioni kufungua kesi kupinga dhamira ya Serikali ya kusaini mkataba huo, kitendo ambacho kilimpa umaarufu sana hasa kwenye mtandao wa X baada ya watu wengi kuunga mkono uamuzi huo.

Siku chache baadae, Nshala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa (TLS) alitangaza kuwa maisha yake yapo hatarini baada ya kuarifiwa kuwa kuna mipango ya kutaka kumuua kwa kulikalia kooni sakata la DP World ambapo wanaharakati walijitokeza kuonya na kukemea huu ya vitisho dhidi ya Nshala. Siku chache baadae Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilimuamuru Wakili Rugemeleza kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, juu ya kauli zake alizozitoa Julai 3.

Ofisi hiyo ilisema kuwa inafanya uchunguzi juu ya kauli alizozitoa, kauli ambazo zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii.

Baada ya kupata intro hiyo (hasa kwa Gen Z wenzangu ambao jina hili lilikuwa geni) uteuzi wa Rugemeleza una maana gani kwa CHADEMA?

View attachment 3213770

Kwa yeyote anayemfahamu Tundu Lissu, bila shaka atakubali kwamba mtindo wake wa siasa, ni mtu ambaye hapepesi macho, si rahisi kuyumbishwa sio kwa vitisho wala kwa rushwa, tabia ambayo tumeiona pia kwa Dkt. Nshala alivyosimama kidete katika kupinga na kupambana dhidi ya mkataba wa DP World.

- Je, kutakuwa na mwanga kwenye ripoti za CAG kuanza kufanyiwa kazi kwa kila anayetajwa kuhusika kwenye ubadhirifu kukaliwa kooni na hatimaye kuchukuliwa hatua?

- Je, siasa za CHADEMA zinaenda kubadilika kutoka kutukanana ovyo na kufanya character assassination na kuwa na vijana wenye kujenga hoja na kuwakabili wapinzani wao kimkakati kutokana na kuzungukwa na viongozi wenye mipango na weledi?

- Je, katika kipindi hiki ambacho, CHADEMA inashikilia msimamo wao wa No Reform, No Election Dkt. Nshala atasaidia kuleta mabadiliko yatakayopelekea kuwa na uchaguzi huru na haki?

Dr Nshala inawezekana ndiyo Mwanasheria kati ya wachache sana aliye msomi kwenye mambo ya rasilimali kuliko wote Tanzania. Ana PHD kutoka shule bora kabisa Duniani
 
Kazingua sana hajaelewa nini huyo?
Yeye mwenyewe kaandika uzi wa hovyo kuhusu Halima Mdee na wale covid wenzake pamoja na Dr Slaa wasirejeshwe CHADEMA mbona tumeheshimu alichokiandika?

Erythrocyte punguza ufia chama na kujiona wewe ni special sana pale inapoandikwa habari kuhusu Chadema na member mwingine
Noma sana, huenda ameuumia sana Mbowe kushindwa bado kamoyo kanachoma
 
Kamati kuu ya Chadema Haina impact yyte ktk nchi hii hao ni nyumbu wanaofanana
Lakini Mama enu jasho linamtoka kwa Lissu kushika usukani! Mwaka huu mtajifunza kitu, Watanzania wa leo sio wa jana🌚🌚
 
Hapanaa, sio Nshala wala TAL anaweza kufanya chochote. Uchaguzi wa 2025 utakuwa huru na wa haki, kwasababu mabadiliko yameisha fanywa na Mama mwenyewe, sheria mpya ya uchaguzi tayari, Tume Huru itaundwa, sasa anakwenda kufanya minimum reforms za katiba.
P
Mkuu unaanza kuwa kama Lucas Mwashambwa siku hizi, unaniangusha Mkuu... tema huo unga wa ndele bwana🥹🥹
 
Dr Nshala inawezekana ndiyo Mwanasheria kati ya wachache sana aliye msomi kwenye mambo ya rasilimali kuliko wote Tanzania. Ana PHD kutoka shule bora kabisa Duniani
Mambo yatakuwa moto, ngoja tuone upepo unavyoenda kuelekea 2025
 
Wakuu,

Januari 21 ulifanyika Uchaguzi Mkuu CHADEMA kwenye nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti kwa Bara na Zanzibar, ambako Lissu alitangazwa kuwa Mwenyekiti mpya CHADEMA, siku hiyo pia ulifanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama na Lissu akafanya uteuzi wa viongozi, na kati ya waliochaguliwa na Mwanasheria wa CHADEMA, Mjumbe wa Kamati Kuu Dkt. Nshala Rugemeleza.

Kwa wale waliokuwa wanafuatilia sakata la DP World jina hili la Nshala Rugemeleza sio jina geni kabisa. Umaarufu wake ulikua zaidi Juni mwaka 2023 alipojitokeza hadharani kupinga mkataba wa DP World kati ya serikali ya Tanzania na Dubai, mkataba ambao aliuita ni “batili” “kiuhaini” na “haramu”.

Nshala hakuishia hapo kwani alitangaza hadharani kuwa yupo mbioni kufungua kesi kupinga dhamira ya Serikali ya kusaini mkataba huo, kitendo ambacho kilimpa umaarufu sana hasa kwenye mtandao wa X baada ya watu wengi kuunga mkono uamuzi huo.

Siku chache baadae, Nshala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa (TLS) alitangaza kuwa maisha yake yapo hatarini baada ya kuarifiwa kuwa kuna mipango ya kutaka kumuua kwa kulikalia kooni sakata la DP World ambapo wanaharakati walijitokeza kuonya na kukemea huu ya vitisho dhidi ya Nshala. Siku chache baadae Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilimuamuru Wakili Rugemeleza kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, juu ya kauli zake alizozitoa Julai 3.

Ofisi hiyo ilisema kuwa inafanya uchunguzi juu ya kauli alizozitoa, kauli ambazo zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii.

Baada ya kupata intro hiyo (hasa kwa Gen Z wenzangu ambao jina hili lilikuwa geni) uteuzi wa Rugemeleza una maana gani kwa CHADEMA?

View attachment 3213770

Kwa yeyote anayemfahamu Tundu Lissu, bila shaka atakubali kwamba mtindo wake wa siasa, ni mtu ambaye hapepesi macho, si rahisi kuyumbishwa sio kwa vitisho wala kwa rushwa, tabia ambayo tumeiona pia kwa Dkt. Nshala alivyosimama kidete katika kupinga na kupambana dhidi ya mkataba wa DP World.

- Je, kutakuwa na mwanga kwenye ripoti za CAG kuanza kufanyiwa kazi kwa kila anayetajwa kuhusika kwenye ubadhirifu kukaliwa kooni na hatimaye kuchukuliwa hatua?

- Je, siasa za CHADEMA zinaenda kubadilika kutoka kutukanana ovyo na kufanya character assassination na kuwa na vijana wenye kujenga hoja na kuwakabili wapinzani wao kimkakati kutokana na kuzungukwa na viongozi wenye mipango na weledi?

- Je, katika kipindi hiki ambacho, CHADEMA inashikilia msimamo wao wa No Reform, No Election Dkt. Nshala atasaidia kuleta mabadiliko yatakayopelekea kuwa na uchaguzi huru na haki?
Chadema ya Lisu ni kete ya dola inayotumika ku neutralize maamuzi mabovu ya chimwaga hivi majuzi!

Ni rasmi Kwa Sasa Tundu ni Raia namba mbili mwenye ulinzi mkali sana ili afanikishe matakwa ya Dola baada ya mwenyekiti kubagaza matakwa hayo ya Katina mpya!

Tuendelee kusubiri hatma ya mwenyekiti was CCM na maamuzi yake!!
 
Hapanaa, sio Nshala wala TAL anaweza kufanya chochote. Uchaguzi wa 2025 utakuwa huru na wa haki, kwasababu mabadiliko yameisha fanywa na Mama mwenyewe, sheria mpya ya uchaguzi tayari, Tume Huru itaundwa, sasa anakwenda kufanya minimum reforms za katiba.
P
Mkuu,
With all due respect, naomba criteria za hiyo tume huru na ya haki itakayosimamia uchaguzi 2025.
 
Wapi imewekwa nongwa Mkuu, ni open discussion, unadhani uteuzi wake utaleta mabadiliko gani CHADEMA na kwenye siasa za TZ kwa ujumla

Afu nimekuaje CCM tena Mkuu?🤔🤔
Tulia mkuu mwenyekiti asuke chama mkuu
 
Back
Top Bottom