LAZIMA NISEME
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 262
- 297
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa kwa wadau wote wa mazingira kuendeleza mambo yoteyaliyofanyika katika maadhimisho ya mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji miti nauanzishwaji wa bustani za kijani.
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya MazingiraDuniani iliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete MkoaniDodoma. Amewahimiza wadau hao kuhamasisha matumizi ya teknolojia za urejelezaji wa taka ozo na za plastiki, kupunguza ukataji miti holela kwa ajili ya kunina mkaa na kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Aidha, Makamu wa Rais amesema Serikali imeweka nia ya kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kwashughuli za kupikia. Amesema katika kutekeleza nia hiyo, Serikali ilitoa katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi yawatu mia moja kwa siku na kuzitaka zihamie katika matumizi ya nishati safi yakupikia ambapo kufikia Machi 2025 jumla ya taasisi 762 zimeanza kutumia nishatisafi ya kupikia kati ya hizo taasisi za umma ni 495 na taasisi binafsi ni 267.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema jukumu la kuhamasisha na kuelimisha jamiikuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira linahitaji ushirikiano wa wadau wote katikangazi zote. ametoa wito kwa vyombo vya habari, taasisi zote za Serikali, binafsi naasasi za kiraia kushirikiana katika kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza uharibifu wamazingira hapa nchini kwa kiasi kikubwa.
Makamu wa Rais amesema taarifa mbalimbali za hali ya mazingira nchinizimedhihirisha kuwepo kwa uharibifu wa ardhi katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo inakadiriwa kuwa takriban asilimia 61 ya ardhi nchini iko katika hatari yakuharibika. Amesema uharibifu huo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu, idadi kubwa ya mifugo isiyolingana na uwezo wamalisho, ukataji wa misitu kwa ajili ya kuni na mkaa, uanzishaji wa mashambamapya unaotokana na kilimo cha kuhamahama, uchimbaji holela wa madini pamojana upanuzi wa makazi usiozingatia mipango miji.
Makamu wa Rais amesema katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira, Serikaliimechukua hatua mbalimbali za kisera na kimkakati ikiwa ni pamoja na kupitishwakwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Mpango Kabambe wa Taifa waHifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032), kuongeza kasi ya upimaji wa ardhina umilikishaji wa ardhi kimila.
Amesema hatua nyingine ni pamoja na uhamasishaji wa matumizi endelevu ya ardhihususan kilimo mseto, kilimo cha matuta, kilimo hifadhi na mbinu endelevu za kiasiliza hifadhi ya malisho. na utekelezaji wa hatua hizi ikiwa ni pamoja na kuendeleakuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Vilevile, Makamu wa Rais amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika UchaguziMkuu wa Rais, Wabunge na Madiwan kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kushiriki kampeni ili kusikiliza sera za wagombea na kujitokeza kupiga kura siku yauchaguzi. Aidha amewasihi wananchi hususani vijana kudumisha hali ya utulivu nausalama hususan katika hatua ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi, upigaji kura na hata baada ya matokeo kutangazwa.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. KhamisHamza Khamis amesema kauli mbiu ya mwaka 2025 inahamasisha jamii kupunguzamatumizi ya bidhaa za plastiki kwa kuwa na uzalishaji na ulaji endelevu kwa lengo la kuhifadhi mito, maziwa na bahari ili kuhifadhi mifumo ya ikolojia.
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa yamebeba kauli mbiu isemayo“Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo, Tuwajibike Sasa: Dhibiti Matumizi ya Plastiki”.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
05 Juni 2025
Dodoma.