Dkt. Philip Mpango, awasili nchini Ufaransa kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa

Dkt. Philip Mpango, awasili nchini Ufaransa kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa

MAKAMU wa Rais wa JMT, Dk. Philip Mpango, amewasili nchini Ufaransa kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika jijini Paris kuanzia leo Jumatano Juni 30 na kumalizika Julai 2, 2021.

Chanzo: Nipashe
Hiki cheo nacho kifutwe kwenye katiba, mbona hakuna Naibu Waziri Mkuu?
 
Maza kasanda
Maza hataki mambo ya kujimwambafai si unacheki siku ametembelea Mwanangamala hospital akaambiwa anaingia ward ya watu wenye matatizo ya kupumua akakimbia zake akawaita wasaidizi eti "nyie tokeni huko, shauri zenu" 😃😃😃😃😃
 
VP? Hii inamfaa Jenista Mhagama.

Inawezekana ktk delegation ya VP yumo pamoja na wanaharakati toka NGOs na maafisa wengine wenye madawati yanayo shughulika na gender equality toka wizara husika, tutawaona ktk siku hizi 3 za forum.

Makamu wa Rais atapewa nafasi kuzungumzia mada hii:

Economic justice and rights
Mete BELOVACIKLI
Sharan BURROW
Winnie BYANYIMA
Maria FLACHSBARTH
Philip MPANGO
Tanzila NARBAEVA
Franz PAASCHE
Julissa REYNOSO
Cyril RAMAPHOSA
Sally ROEVER
Guy RYDER
Pedro SÁNCHEZ
Violet SHIVUTSE
Preeti SINHA
Sofia SPRECHMANN
SINEIRO
Mr. Mark SUZMAN
 
MAKAMU wa Rais wa JMT, Dk. Philip Mpango, amewasili nchini Ufaransa kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika jijini Paris kuanzia leo Jumatano Juni 30 na kumalizika Julai 2, 2021.

Chanzo: Nipashe
Bado napata na wasiwasi na afya yake...
Mbona kama bega moja limeshuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
30 June 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango jana Juni 29, 2021 amewasili Paris nchini Ufaransa ambako atahudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa kuanzia Juni 30 – Julai 2, 2021.

Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo.

Aidha, Makamu wa Rais alipata maelezo jinsi Ubalozi wa Tanzania unavyotekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi katika eneo lake uwakilishi ambalo ni Ufaransa, Hispania; Ureno; Algeria na Morocco.

Maelezo hayo yalitolewa na Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Pia Balozi Shelukindo anaiwakilisha Tanzania katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amempongeza Balozi Shelukindo kwa uwakilishi mzuri katika nchi hizo na kumuhakikishia serikali itaendelea kutatua changamoto zinazojitokeza katika ubalozi huo. Amemtaka kuendelea kutafuta mahusiano na sekta binafsi zilizopo nchini Ufaransa kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Leo juni 30,2021 Makamu wa Rais anatarajia Kuhudhuria ufunguzi wa Jukwaa la kizazi cha usawa lenye lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 1995.
Source : Daily News digital
 
Maza hataki mambo ya kujimwambafai si unacheki siku ametembelea Mwanangamala hospital akaambiwa anaingia ward ya watu wenye matatizo ya kupumua akakimbia zake akawaita wasaidizi eti "nyie tokeni huko, shauri zenu" 😃😃😃😃😃
Nurses anataka wafe yeye abaki
 
Back
Top Bottom