Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Wahenga wanasema tembea uone. Ndio maana hata mzee Mwinamila alipokuwa hai aliwahi kutunga wimbo akimwambia Mwl Julius Nyerere atembee aone ili ajionee kwa macho yake nchi anayoitawala na watu wake wanaishi kwa namna gani.
Nimepafanya kijiziara kidogo suo moto, maana sijapangiwa na mtu. Ila nimeshuhudia kuwa watanzania bado wana hali mbaya sana kiuchumi. Watanzania wanaishi maisha duni, kula ni kwa tabu,kulala kwa tabu kwa kweli inasikitisha sana.
Ukweli ni kwamba watanzania sio wavivu, wanapenda kazi, maana nimeshuhudia kwa macho yangu, wanalima, wanachimba madini tena kwa mikono, wanafanya biashara. Kwa ujumla wanajituma japokuwa wapo baadhi ni wavivu na matapeli.
Lakini huu umaskini unatoka wapi? Fikiria mama ana mtoto mgongoni anajishughulisha kuosha vyombo kwa mama ntilie na analipwa shilingi elfu mbili, kwa jinsi pesa isivyo na thamani ataishi vipi?
Dkt. Mpango siku unaapishwa ulikiri kwa kinywa chako, ulipokuwa unafanya kampeni umeshuhudia umaskini mkubwa sana wa wananchi wa jimbo lako. Na ukweli ni kuwa hali uliyoishuhudia ndio hali halisi ya watanzania 75%.
Dkt. Mpango kama mchumi, unatusaidia vipi sisi watanzania kuepukana na hii hali? Je, huwa unamueleza ukweli mkuu wa nchi juu ya hii hali uliyoishuhudia? Una mpango gani wa kuleta sera nzuri za kiuchumi kuwaokoa hawa watanzania wanaoteseka?
Au uliongea kama unajikosha tu mbele ya umma,maana hatuoni ukichukua hatua ili kutunusuru.