Dkt. Philip Mpango: Tusikae kulalamika kuwa viongozi hawafanyi kazi bila juhudi za kuwachagua

Dkt. Philip Mpango: Tusikae kulalamika kuwa viongozi hawafanyi kazi bila juhudi za kuwachagua

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango, ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, katika Kanisa la Mt. Francis Xavier, Nyakahoja, Mkoa wa Mwanza.

Katika hotuba yake, Mpango amewahimiza wananchi kujiandikisha kwa wingi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika Novemba 27. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wananchi kuchukua hatua ya kujitokeza na kujiandikisha ili kuchagua viongozi wenye uwezo. "Tusikae kulalamika kuwa viongozi hawafanyi kazi ikiwa hatujafanya juhudi za kuwachagua" alisema Mpango, akihamasisha uwajibikaji miongoni mwa raia.

Pamoja na hayo Dkt. Mpango amesisitiza wananchi wenye sifa za kuongoza hasa wanawake kujitokeza na kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi "nawaomba sana wale wenye uwezo wa kuongoza wajitokeze na hususani akina mama ambao mnajua shida za akina mama wenzenu lakini najua mnajua shida zetu akina baba pia"

Soma: Dkt. Philip Mpango: Wanawake jiandikisheni uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mchukue fomu kugombea uongozi
 
Back
Top Bottom