GE2025 Dkt. Saada Mkuya: Ukienda kufanya vurugu siku ya Uchaguzi, bima haitakulinda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Your browser is not able to display this video.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amewataka Watanzania kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu, akisisitiza kwamba bima haziwezi kumlinda mtu anayejiletea madhara kwa makusudi kutokana na kushiriki vurugu wakati wa uchaguzi. Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), tukio lililoambatana na uwasilishaji wa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa mwaka 2024, Dkt. Mkuya amesema ni jukumu la kila raia kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani bila uvunjifu wa sheria.

“Uchaguzi bila ya vurugu inawezekana. Ukiwa unakwenda kufanya vurugu, bima haitakulinda, kwa sababu utakuwa umetafuta jambo la makusudi. Tunaomba sana ushiriki uchaguzi huu kwa sababu ni haki yako kikatiba, lakini uchaguzi huo tukaushiriki kwa amani na utulivu,” amesema Dkt. Mkuya.

Waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha sekta ya bima inakuwa imara na inawanufaisha wananchi wote, huku akihimiza Watanzania kuendelea kujiunga na huduma za bima kwa maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
 
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amewataka Watanzania kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu, akisisitiza kwamba bima haziwezi kumlinda mtu anayejiletea madhara kwa makusudi kutokana na kushiriki vurugu wakati wa uchaguzi.

Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), tukio lililoambatana na uwasilishaji wa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa mwaka 2024, Dkt. Mkuya amesema ni jukumu la kila raia kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani bila uvunjifu wa sheria.

“Uchaguzi bila ya vurugu inawezekana. Ukiwa unakwenda kufanya vurugu, bima haitakulinda, kwa sababu utakuwa umetafuta jambo la makusudi. Tunaomba sana ushiriki uchaguzi huu kwa sababu ni haki yako kikatiba, lakini uchaguzi huo tukaushiriki kwa amani na utulivu,” amesema Dkt. Mkuya.

Waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha sekta ya bima inakuwa imara na inawanufaisha wananchi wote, huku akihimiza Watanzania kuendelea kujiunga na huduma za bima kwa maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
Your browser is not able to display this video.
 
Maandamano ni ya watanganyika na sio wazanzibar ashughulike na asili yake huko
 
BIMA siyo bure, mbona mtu asipoitumia mpaka inapo expire harudishiwi pesa...
Na ndiyo hivyo hivyo kwa hali yoyote ile inapaswa atibiwe...


Cc: Mahondaw
 
Anamdanganya Nani ??saizi bima ya afya haifanyi kazi !!
 
Huyu amekuwa msemaji wa Bima ya Afya?.🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…