Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Katibu wa Siasa na Unezi wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoani Njombe ndugu Ally Nathan Mhagama ( Dk Saga Saga) Agosti 10,2025 amekutana wananchi wa Vijiji vya Ugera na Mkongobaki wilayani Ludewa Mkoani Njombe kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo na kuomba ridha ya kugombea nafasi ya Ubunge.
Akizungumza na wananchi ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wote wa wilaya ya Ludewa kupokea ombi hilo nakusisitiza kwamba hitaji lake nikuhakikisha anasaidia kusukuma mbele guruduma la maendeleo katika suala la mradi wa makaa ya mawe wa Liganga na Mchuchuma, kushughulikia miundombinu ya barabara Kilimo na Elimu.
Licha ya kuhakikishiwa nafasi ya Udiwani na wananchi hao Ally Mhagama amewasihi kufahamu kwamba wanapaswa kuungana pamoja na kushughulikia changamoto za Ludewa nzima ikiwa ndilo kusudio lake kuu kwani amepokea wito toka kwa wananchi wa Kata zote zaidi ya 20 wilayani wakimsihi kugombea nafasi hiyo.