Dkt. Salim Ahmed Salim atimiza umri wa miaka 80. Mungu mpe maisha marefu

Dkt. Salim Ahmed Salim atimiza umri wa miaka 80. Mungu mpe maisha marefu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
01568225-7467-4D3B-B10B-F63FF38D5E11.jpeg

Leo tarehe 23/01 /2022 Mzee Salim Ahmed Salim anatajwa kutimiza miaka 80 tangu kuzaliwa kwake, hii ni baraka kubwa kwake na kwa familia yake.

Sisi wengine tunamtakia heri ya siku hii mzee wetu huyu ambaye ni miongoni mwa Watanzania wachache WALIOILETEA HESHIMA NCHI YETU.

FUNZO: UKIWA NA ROHO NYEUPE UTAISHI MAISHA MAREFU , BALI UKIWA NA ROHO MBAYA , UKATILI , WIVU NA KISOKOLOKWINYO UTAKUFA MAPEMA TU
 
Mungu amzidishie afya na nguvu Mwana Diplomasia nguli wa Afrika mashariki.

Ukiwa mwema kwa Taifa lako na Mzalendo wa kweli basi utapata amani ya roho na mwili.
lakini ukiwa mharibifu wa amani ya Taifa lako basi tambua utapata taabu sana hadi mwisho wa maisha yako.

Nawaasa watanzania wote tuipende nchi yetu, tuwe wazalendo wa kweli ili wananchi watuheshimu daima na milele.
 
Hawa ndio watu ambao wakifa miwili Yao ikitembezwa na kuzungushwa nchi nzima sawa tu.

Lkn eti linakufa jitu liuaji libambikiaji kesi, litekaji mnatusumbua barabarani.

Mtu kama Maalim amekufa watu wanaenda kufanya hija alipozikwa huyo ndio muungwana mzalendo na mcha Mungu.

Mlitusumbua sana na aliyefia pale vichochoroni makumbusho/ Mzena
 
Je asili yake ni wapi. Nasikia anatokea pemba ndo sababu zilizomfanya akaukosa urais zanzibar
 
Laiti nchi yetu, wakati wote ingebahatika kuwapata viongozi wa namna ya Salim Ahmed Salim, hakika, nchi yetu isingekuwa duni kama ilivyo leo.

Kuna nyakati nchi imekuwa inaongozwa na watu ambao ni majambazi, wauaji, watesaji, majizi, majitu yasiyo na weledi wowote kuhusu uchumi. Majitu yanayodhani ukipata madaraka au cheo, kazi yako ni kuswaga watu kama ngiri.

Happy birthday Salim, ujaliwe maisha marefu yenye heri, furaha na amani.
 
Wazungu wanasema ni missed opportunuity. Tuliipoteza na haitatokea tena...
Laiti nchi yetu, wakati wote ingebahatika kuwapata viongozi wa namna ya Salim Ahmed Salim, hakika, nchi yetu isingekuwa duni kama ilivyo leo.

Kuna nyakati nchi imekuwa inaongozwa na watu ambao ni majambazi, wauaji, watesaji, majizi, majitu yasiyo na weledi wowote kuhusu uchumi. Majitu yanayodhani ukipata madaraka au cheo, kazi yako ni kuswaga watu kama ngiri.

Happy birthday Salim, ujaliwe maisha marefu yenye heri, furaha na amani.
 
Yesu Kristu alifariki na miaka 33.

Martin Luther King Jr. alifariki na miaka 39, Malcom X alifariki na miaka 39.

Rais John F. Kennedy alifariki na miaka 46.

Mtume Mohammad S.A.W. alifariki na miaka 61-62.

Bila shaka hawa wote walikuwa na visokorokwinyo!!!
 
Back
Top Bottom