Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, unaopita Singida, utakuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wa eneo hilo na Watanzania kwa ujumla.
Mradi huu wa kimkakati, ujulikanao kama East African Crude Oil Pipeline (EACOP), unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja katika ujenzi na huduma za kiufundi, huku biashara ndogo ndogo za chakula, malazi na usafiri zikifunguka kwa wananchi wa Singida.
Zaidi ya ajira, bomba hili litaongeza mapato ya serikali na kuchochea maendeleo ya miundombinu, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kikanda kati ya Tanzania na Uganda.
Kauli ya Rais Samia imeibua matumaini mapya kwa vijana wa Singida, ambao sasa wanahimizwa kujiandaa na kuchangamkia fursa zitakazojitokeza. Mradi huu si wa serikali pekee, bali ni urithi wa maendeleo kwa wananchi wote.