BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi leo amechangia Bajeti ya Wizara ya TAMISEMI Bungeni Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ametoa hoja mbalimbali kwa ajili ya kutatua kero na kusukuma maendeleo Jimboni kwake.
Kwanza; Dkt. Samia amempongeza Rais Samia kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambapo Jimbo la Muhambwe katika mwaka huu wa fedha limepata Bilioni 18 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Pili; ameieleza Serikali changamoto ya ajira na uhaba wa watumishi katika sekta ya elimu na afya Jimboni kwake akiomba Serikali itatue changamoto hii kwa haraka ili wananchi wapate huduma bora zaidi.
Tatu; ameeleza changamoto ya uhaba wa watumishi kwa walimu wa shule za msingi na sekondari akiomba walimu kuongezwa.
Nne; ameomba shule za kidato cha 5 na 6 kuongezeka kutoka 3 zilizopo sasa hadi 5 lakini hata zile 3 zilizopo Serikali iongeze madarasa maana bado kuna changamoto kubwa ya madarasa. Pia amemuomba Waziri afike Kumkugwa sekondari ya kidato cha 5 na 6 ambayo ilikuwa kambi ya wakimbizi ajionee uchakavu na uhaba wa miundo mbinu ya madarasa
Tano; aomba Serikali kupitia TARURA kujenga barabara ili kuunganisha barabara za Jimbo ili kuharakisha shughuli za wananchi.
Sita; mahitaji ya madaraja ya mawe yaongezeke haraka kutatua kero hii Jimboni.
Saba; kumalizia maboma ya zahanati na kumalizia madarasa.
Nane; mwisho, Dkt. Samizi amemalizia kwa kuitaka Wizara ya TAMISEMI kutekeleza ahadi za Viongozi wa Juu wa Nchi walizotoa Jimboni ikiwemo kumalizia maboma ya vituo vya afya, zahanati na madarasa kama boma la kituo cha afya Kizazi.