GE2025 Dkt. Shein, Karume wampongeza Rais Mwinyi kwa ushindi, kudumisha amani

GE2025 Dkt. Shein, Karume wampongeza Rais Mwinyi kwa ushindi, kudumisha amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amekutana na marais wastaafu wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Shein wa awamu ya saba na Amani Abeid Karume wa awamu ya sita, Ikulu Zanzibar jana Jumamosi, Novemba 8, 2025.
1762681696313.png
Marais hao wastaafu wamemtembelea Rais Mwinyi kwa lengo la kumpongeza kwa ushindi wa kishindo alioupata, pamoja na kupongeza hali ya amani na utulivu iliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu.

Soma: ZEC yamtangaza Dk Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzaibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilimtangaza Dk Mwinyi kuibuka mshindi wa urais kwa kupata kura 448,892 sawa na asilimia 74.8.

Dk Mwingi aliwashinda washindani wake wengine 10 aliokuwa akichuana nao akiwamo Othman Masoud Othman ‘OMO’ kutoka ACT Wazalendo ambaye alipata kura 139,399 sawa na asilimia 23.22.

Kwa mujibu wa ZEC, waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 717, 557 lakini waliopiga kura walikuwa 609, 096 sawa na asilimia 84.88. Kati ya kura hizo zilizoharibika ni kura 8,863 sawa na asilimia 1.46.
 
Huyo wa kulia kabisa mbona kaa halipwi kiinua mgongo.
 
Hilo la kupongezana halituhusu Watanganyika
Hako ni ka nchi jirani tu!

Sisi tuna jambo letu 9dec tukutane.
 
Back
Top Bottom