Mzalendo ni yule anayetaka tuwe na taasisi imara zinazofanya kazi kwa weledi.Unasema unapinga udini na vyama kuwa mbele ya maslahi ya taifa lakini wakati huo huo unaitetea taasisi ya usalama inayotanguliza maslahi ya chama mbele na kutumika kupandikiza mbegu za udini kwa maslahi ya kisiasa na kushindwa kutoa ushauri makini kwa rais.
Taasisi ambayo inamuelekeza waziri kwenda kutoa tamko juu ya nani achinje?
Taasisi iliyoruhusu fedha za EPA zichotwe na kutumika kwenye kampeni za uchaguzi kwa chama tawala huku wakishindwa kumshauri rais juu ya umuhimu wa kufuata utawala bora wa sheria ili wahusika waburuzwe mahakamani badala yake Rais akawaambia warudishe.Ni picha gani hii iliyojengwa kwa vibaka wa mitaani?
Kwamba unasema tukubali ushauri?Nitakishangaa CHADEMA kama kitakubali kila ushauri hata ule wa kipumbavu,tutakua hatuna tofauti na watawala tulio nao wanaoshauriwa kutoa maagizo ya kiserikali kwenye masuala ya dini na kusamehe wazi wa mali za umma.
CHADEMA kinapenda ushauri wenye tija ndiyo maana kuna kitengo cha utafiti na sera ambacho kinaongozwa kwa weledi.Professional consultancy ni nguzo kuu katika utendaji wake hasa yale yanayohitaji professionalism.Make no mistake!
Hilo la CHADEMA kuchukua madaraka linakutisha sana unaandika kwa jazba.Mtaumia wengi ila ni suala la muda tu....na bado.
Nduka,
Hebu soma kwa sauti kubwa hicho ulichoandika hapo.Sometimes it's better to be silent kuliko kujidhalilisha hata kama unatumia ID fake