Dkt Slaa aligawa Bunge


Thanks for highlighting that. Every Government has a law in classified Documents. Since the wake of Ufisadi, there has been a lot of reports and documents that have revealed the truth about Ufisadi, now would you really classify the UFISADI documents as sensitive data that could jeopardize the security of the country. I think there is a level of sensitivity that requires one to receive clearance of having such documents. But so far, I think it is quite embarrassing to hear these wabunge trying to rally against Dr. Slaa. You would think as a member of parliament representing TZ people, he would have the right to certain documents. It is about time we all have to unity against such wabunge jamani.
.
 
Wakati umefika kwa Tanzania kuwa na wabunge wa kujitolea badala ya kuwa na wawakilishi wanaokwenda bungeni kuchuma. Wabunge wamefikia hatua ya kumnyanyasa Dr Slaa ati kwa sababu kasema ukweli kuwa analipwa mishahara mikubwa, wanataka iwe siri yao. Inatosha, tupate wabunge wa kujitolea ambao kweli watakuwa wanatetea maslahi ya wananchi badala ya kuganga njaa zao na kujitarisha. Mnaonaje wana JF?
 

Siku ikitangaza kwamba ubunge nikujitolea, nadhani hakuta kuwa na mbunge hata mmoja kila mtu atakimbilia kwenye kibarua chake!

Any way this is a good wishfulthinking!
 


Wananchi wa majimbo ya wabunge hawa mnataka nini tena?! Mmeshajua aina wa wabunge mlio nao. mnafikiri wanawajali hawa? 2010 hawatakiwi kuendelea na ubunge hawa. Wao wanashughulikia matumbo yao tu- kupitisha nyongeza za ajabu za mishahara yao tu huku walimu, mapolisi na walala hoi wengine wakikosa hata mlo wa siku!? kweli tunawahitaji wabunge wa namna hii?

Hivi kutoa uthibitisho wa EPA, RADA, Twin towers na ufisadi mwingi mwingine ni kutoa siri za serikali? BASI BUNGE LINATAKIWA LIBADILISHE SHERIA INAYOWABANA WABUNGE KUTOA HOJA ZA KWELI NA ZENYE VITHIBITISHO. Mbunge atakapo toa vithibitisho kuhusu hoja inayoihusu serikali kwa vyovyote hivyo vithibitisho vitakuwa nyaraka za serikali na pengine za siri.

Serikali iache kutuzingua hapa - kama hutaki moshi uonekane nje basi usiwashe moto mnasema siri za serikali huku zinahusu kuhamisha fedha za walala hoi kwenda kwa mafisadi na ccm. wizi mtupu!
 
Jibaba Bonge

Heshima kwako... Labda tukisema wananchi waing'oe CCM yote katika uchaguzi ujao ni sawa na kuifukuza mvua kwa makelele!

Naungana nawe, wanachi wa majimbo ya wabunge hawa (Singida Kaskazini, Nkasi na Kibakwe) mna dhamana kubwa kwa taifa letu. Hebu tuondoleeni bootlickers hawa. Tusiwaone tena kwenye bunge lijalo.
 
Sijui Tz ya sasa bila Dr. Slaa ingekuwa ktk hali gani! Amost single-handed he is fighting for us (naturally docile/coward? people)
 
Usikate tamaa Dr. Slaa, na tutaendelea kukupa data zingine hata ziwe za siri hadi serikali itakaposimamia na kukomesha Ufisadi
 
...unategemea nini kuwa na wabunge kama kina Nyalandu mtu aliyepata ubunge kwa kujipendekeza,anachojua ni utapeli tuu na ass kissing ili maisha yake yaende mbele!
 
Hatuwezi kusema kuwa wabunge wote wa CCM ni wabinafsi na wanaopenda 'siri' kushabikia uhujumu wa nchi unaofanywa na viongozi wachache wa serikali.

Bunge halipaswi kuisemea serikali na hapa ndo dhana ya mgawanyo wa madaraka unapoonekana.

Kwa walio nje ya nchi na wanaojua kzungu, pana mambo mengi sana ambayo huku tulikuwa tunajua ni siri lakini baadhi ya mataifa makubwa na raia wake walikuwa wanajua hadi kilicho ndani ya bukta ya tanzania.

dr Slaa hawawezi kunyamazishwa na watu wenye kupenda kupewa madaraka kwa kusema upuuzi kama hao walionukuliwa na Majira.

Watu kama kina Nyalandu kutokana na maovu yao waliyofanya kwa jamii wanadhani kila kitu kinaweza kuwa siri. hakuna siri mbele ya maslahi ya umma


SIRI HAIHUSISHI WENGI, TUMEWAGUNDUA MAFISADI JAPO CCM ILIFANYA SIRI
 
Huu mkuu ni ukweli usiofichika.

Naona pale wanakula per deam tu. Hata hoja wanazoziridhia sidhani kama sinapitiwa kwa undani. Maswali yanayoonyesha kwamba wabunge wanaaply crirical thinking hamna kabisa.

Bunge letu Michosho sana.
Herbert,
Ulichosema ni sahihi kabisa. Juzi mimi na wenzangu wachache tulifanya utafiti mdogo ndani ya Ukumbi wakati wa Bunge zima. Tumegundua kitu cha ajabu sana, na tusipoangalia kitapeleka nchi shimoni kabisa. Kati ya Wabunge 150 waliokuwa ukumbini, ni wabunge wasiozidi 30 walikuwa na Mswada. Wengine wote, na hasa waliokuwa wanapaza sauti kusema "Ndiyo" kupitisha vifungu walikuwa hawana kabisa vitabu, na hivyo ni vigumu kuamini kuwa walikuwa wanafahamu vifungu vyote vilivyokuwa vikipitishwa. Kilichoonekana au ni kupitisha vifungu na muda upite, au kuvipitisha kwa vile mswada umeletwa na Serikali yao. Kwa vile Bunge liko live siku hizi, ni vema waandishi wa Habari walioko kwenye JF nao pia watusaidie. Inawezekana siri ya nchi yetu kupitisha Sheria zisizo na maslahi kwa wananchi, au zinazokinzana ni kutokana na hali hii ya Wabunge kutokusoma miswada inayowasilishwa Bungeni na kuzipitisha kimzaha mzaha tu. Nimestuka sana na hali hii, na hiwezi kuachwa bila kukemewa. Tusaidiane kufanya utafiti ili tuweze kuikemea vizuri. Mapenzi kwa nchi, yanaanzia kwa kutunga sheria nzuri. Sheria nzuri hutungwa na wabunge makini.
 


Dr. Slaa you are very right, ni kweli Baadhi ya wabunge huwa wanajibu kitu bila kusoma na bila kuelewa nini kimo ndani, ili mradi kimetoka kwenye Chama chake tu.

Nakumbuka wakati Waziri wa elimu wakati huo Mungai alipeleka bungeni mabadiliko ya mitaala ya secondary na kufuta masomo ya kilimo na ufundi, wabunge wa upinzani waliona hilo lakini wale wa CCM walipitisha bila kuhoji. Miaka miwili baadaye tumeshuhudia wabunge wa CCM wakimhoji Mungai kuwa nani alimtuma kufuta masomo na michezo mashuleni!!!!, naye aliwajibu kuwa ni Ninyi ndiye mliopitisha budget yangu na ilikuwa na hayo mabadiliko!!! wengi walibaki wametoa mimacho. Na hilo ni kutokana na kutosoma kilichomo na kubaki wanasinzia bungeni, wakiamka wanaangalia nani kaleta mswada kama ni chama chake basi Ndiyoooooo!!

Kweli hatutafika kwa mtindo huo, ni vyema tuanze kupigia kelele ili wabadilike
 
Someni hapa Dk. Slaa: Sitishiki

Inaudhi sana, hawa wawakilisha matumbo badala ya wananchi tulio watuma dawa yao inachemka jikoni, kama alivo sema mpambanaji Slaa tuna wasubili 2010, tutakula nao sahani moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…