Risk taker
Member
- Jan 20, 2009
- 35
- 0
ONYO lililotolewa na Serikali kwa Wabunge juzi kutothubutu kutumia nyaraka muhimu za Serikali kama kithibitisho katika kujenga hoja mbalimbali Bungeni, limechukua sura mpya baada ya wawakilishi hao wa wananchi kugawanyika juu ya uamuzi huo.
Mgawanyiko huo umetokana na baadhi ya Wabunge wa CCM kuitaka Serikali kumchukulia hatua za kisheria haraka Mbunge wa Karatu Dkt. Wilbrod Slaa (CHADEMA) na kueleza kwamba hawatarajii kuona akiachwa hivi hivi, huku baadhi ya pia wakitofautiana na wenzao na kumuunga mkono Dkt. Slaa kwa maelezo kwamba onyo la Serikali ni vitisho vinavyolenga kuwaziba mdomo Wabunge kuelekea uchaguzi Mkuu 2010.
Wabunge watatu wa CCM, Bw. Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini), Bw. Ponsiano Nyami (Nkasi) na Bw. George Simbachawene (Kibakwe) walisema wanaungana na Serikali na kwamba hatua ya kutoa onyo imechelewa kwa maelezo kwamba tayari tabia hiyo imeiletea nchi dosari kubwa mbele ya Mataifa mengine ya nje.
"Kwanza kabisa Serikali imechelewa kuchukua hatua na hata hivyo hatutarajii kuona akiachwa hivi hivi. Tunataka Serikali imchukulie hatua za kisheria haraka aliyekwishahusika na hilo kosa, tayari tumepata athari watu wa nje wanatuona kama watu waliochanganyikiwa," alidai Bw. Nyami akiungwa mkono na wenzake wawili.
Naye Bw. Simbachawene alisema amesikitishwa na hali hiyo na kueleza kwamba chanzo cha tatizo hilo ni hulka ya Watanzania ya kuvumiliana, busara na hekima inayotumiwa na viongozi kutoharakisha kuwachukulia watu hatua wakitaka Watanzania waendelee kuishi kwa amani na utulivu na kuamini kwamba kila mtu akitambua hilo hawezi kufanya kile kilichofanywa na baadhi ya Wabunge kutoa siri za Serikali hadharani.
"Kinachofanywa na Dkt. Slaa ni kutaka kuichanganya Serikali kwa ujumla ili ifikie wakati wananchi wakose imani na Serikali yao jambo ambalo ni hatari sana kwa Taifa. Anataka kutufanya kama watu wote waliochanganyikiwa, hatuwezi kukubali, Mbunge ana njia nyingi za kuishauri Serikali si kutoa siri za nchi tena kwenye mkutano wa hadhara," alidai Mbunge huyo.
Naye Bw. Nyalandu alidai Mbunge kuweka hadharani nyaraka za siri za Serikali katika mkutano wa hadhara ni aibu kwa Taifa kubwa na lenye sifa
njema kama Tanzania na kwamba haliwezi kuvumiliwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Bumbuli (CCM), Bw. William Shellukindo alisema kitaratibu zipo nyaraka za Serikali ambazo haziwezi kuwa wazi hadi kufikia kipindi cha miaka 20 au zaidi na kwamba ikibainika umezitoa unaweza kuchukuliwa hatua kali hivyo anaungana na Serikali kuhusu onyo hilo.
"Mimi nimefanya kazi Serikalini muda mrefu, zipo nyaraka za siri ambazo haziwezi kuwa hadharani mpaka miaka 20 ya muda fulani, ukibainika umezitoa unastahili kuchukuliwa hatua za kisheria. Naungana na Serikali kabisa," alisema Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.
Kwa upande wake kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Bw. Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema kinachotakiwa kwa Serikali ni kushughulikia chanzo cha tatizo badala ya kuwatishia wabunge na kuwajengea hofu wananchi kuhusu taarifa za kweli kuhusu vitendo vya ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka serikalini.
"Ushauri wangu kwa Serikali ni kushughulikia ufisadi badala ya kutishia Wabunge na kutaka kujenga hofu kwa wananchi. Kama ikishughulikia tatizo la ufisadi na kika kitu kikawa wazi utahitaji nyaraka za nini?" Alihoji Bw. Hamad.
Kuhusu taarifa za siri zinazotokana na nyaraka Serikali kujulikana kwa watu wa nje, Bw. Hamad alisema anayedhani wapinzani ndio wamevujisha siri hizo kwa watu wa nje hana upeo mpana wa kuelewa kwa kuwa mataifa ya nje wana taarifa za siri za ufisadi wa Tanzania kuliko hata Watanzania na kuongeza kwamba hata wapinzani wanapata siri nyingine nje ya nchi.
"Nataka nikuhakikishe kwamba hata siri ya ubadhilifu katika Wizara ya Maliasili na Utalii zimeibuliwa na nchi moja kubwa ya nje. Sisi tunapata taarifa nyingi sana nje na kushangaa kwamba kumbe nchi za nje zinajua siri za matumizi mbaya ya madaraka ya nchi yetu kuliko hata sisi Wabunge," alisema Bw. Hamad.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutoatajwa majina baadhi ya Wabunge wa CCM walionesha masikitiko yao kwa Serikali kutoa onyo kwa kwao kuhusu nyaraka muhimu na kudai kuwa hilo si dawa katika nchi ya demokrasia kama Tanzania.
Walisema hatua iliyokwishaanza kwa Bunge kutekeleza wajibu wake haitakiwi kutiwa dosari kama ambavyo Serikali inavyotaka kufanya na kwenda mbali zaidi wakidai huenda baadhi ya mafisadi wameanza kuwazidi nguvu baadhi ya watendaji wa Serikali na kukubali hoja zao za kutaka kukitaka Serikali kulegeza kamba katika vita dhidi ya ufisadi.
SOURCE: MAJIRA