KWELI Dkt. Slaa asema amepata taarifa kuwa Deusdedith Soka atauawa na kutupwa msituni

KWELI Dkt. Slaa asema amepata taarifa kuwa Deusdedith Soka atauawa na kutupwa msituni

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari wapendwa, kuna taarifa inatembea mitandaoni kuwa Dkt. Slaa amepata taarifa ya Deusdedit Soka ya kwamba atauawa leo na kutupwa msituni, je, Taarifa hiyo ni kweli imetoka kwa slaa? Na ina ukweli?

1724316294963.png

 
Tunachokijua
Deusdedith Soka ni Mwenyekiti wa Vijana Temeke kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Mnamo tareheAgosti 8, 2024 alitoweka na mpaka leo tarehe 22,08,2024 haijafahamika alipo licha ya jitihada za watu mbalimbali na chama chake kuendelea kumtafuta alipo.

Taarifa ya CHADEMA kuelezea tukio hili imehifadhiwa hapa.

GVbvG7kWUAA62PC
Mnamo tarehe 21, Agosti 2024, zilianza kusambaa taarifa zilizodai kuwa ni taarifa kutoka kwa Dtk. Wilbroad Slaa ambaye alidai amepata taarifa kuwa Soka atauawa usiku wa tarehe 21, 08, 2024 kabla ya saa 8 usiku na kutupwa kwenye msitu na kwamba hiyo ni amri imetolewa. Tazama

Jamiicheck, Imemtafuta na kuzungumza na Dkt Slaa ili kupata uhalisia wa taarifa hiyo ambaye amekiri kuwa ni kweli ujumbe huo ni yeye ameutoa na taarifa hizo ana uhakika nazo.

"Jana majira ya saa 10 jioni nilipokea taarifa kutoka kwenye vyanzo vyangu vya kawaida, kuhusu kijana wetu ambaye ni Soka, Soka ni kijana ambaye namfahamu nimewahi kufanya naye kazi mara kadhaa namfahamu namna anavyofanya kazi zake na mara kadhaa mekuwepo kwenye press coference zangu, namfahamu kwa undani, nafahamu nia yake kwa Tanzania, namfahamu namna ambavyo anavyolipenda taifa lake ambalo ni Tanzania.

Ni dhahiri ukipata taarifa kama hiyo ya mtu unayemfahamu kuwa leo usiku maisha yake yatafika mwisho leo usiku, nilistuka sana, kwa hiyo nikawashirikisha viongozi wa sauti ya mtanzania. Na tukafanya mkutano na kuweka maazimio juu ya jambo hilo.

Hili sio jambo ambalo tungeweza kukaa nalo, hivyo tukaweka maazimio juu ya namna ya kuwajulisha watanzania kupitia sauti ya Mtanzania.

Watu waliopewa kazi ya Kufikisha mwisho maisha ya Soka ndio haohao walioshughulika na Sativa, na wanajulikana majina yao, Hivyo nilipopata taarifa hiyo nikaona ni vyema kuwajulisha watanzania. Hao ndio waliohusika na mchakato wa kumkamata ikiwamo yule msichana ambaye anatembea na bodaboda, ni msichana, mwanamke mweupe umri wa makadirio ni miaka 20 kwenda 30 ambaye huwa anatembea na bodaboda, ni mwanamke hatari kwa kuwa yeye ndiye ambaye huwa anaweka mitego ya kuwakamatisha ambao hao wote ambao huwa wanakamatwa.

Katika hatua hiyo, picha tuliyoambiwa usiku huo ni kwamba walikuwa wanaondokea pale kwenye kituo cha polisi pale cha Mikocheni, cha Osterbay kwa hiyo watawapeleka kwenye uelekeo ambao wamepangiwa , uelekeo hasa ni upi kati ya Tanga na Arusha hatukua tunajua ila ilibidi tupate taarifa kwa wakati huo, na baada ya hapo watu wetu watajadili kama ambavyo wamekuwa wakijadili mambo yetu.

Kwa sasa watanzania tumefikishwa mwisho wa uvumilivu, kama wanaweza kutunzwa ndani ya vituo leo anaweza kuwa Soka kesho ni mwingine.

Labda nikukumbushe namna ambavyo Soka alikamatwa safari hii, Soka alikamatwa kwa kuitwa kwenda kituo cha polisi kutambua pikipiki yake ambayo mwaka jana polisi Waliikamata na haikurudishwa mpaka leo wala kupigiwa simu. Kwa hiyo alipoitwa hakuwa wala na wasiwasiila kwa tahadhari ya kawaida alichukuzana na rafiki yake wa kawaida walikwenda pamoja na mbele ya rafiki yake alichukuliwa tu akawekwa ndani na rafiki yake akaachiwa.

Na ndio sababu ya watu kuwa na wasiwasi kama ambavyo sasa hivi kuna vituo vinavyoitwa vya gereji, Kama mmewahi kusoma kitabu cha Mdude Nyagali ambacho aliandika baada ya kushinda kesi ya kukutwa na madawa ya kulevya na mahakama kuthbisha kuwa Polisi ndio walimuwekea Mdude madawa ya kulevya hivyo huo ni uthibitisho wa yanayotokea vituoni, Tulidhani Sativa atakuwa mtu wa mwisho kupotea, ila sasa Aliyechora picha ya Rais na kuichoma naye haonekani na sasa Soka sasa ndio maana hii taarifa tuliona kuna umuhimu wa kulishughulikia na tumepeleka taarifa kila sehemu ikiwemo mabara mbalimbali.
Dkt Wildroad Slaa Akizungumza na Jamiicheck
Bendera zenye rangi nyeusi katikati zina matatizo sana.
 
Nchi hii imejaa dhulma kila kona ndio maana hatupati maendeleo.
 
Tarehe 21/08 ishapita saa 8 ishapita tuanze kuutafuta mzoga sasa kwenye hio misitu ya karibu km utapatikana au sio hivyo?
 
Inaonekana ofisi za mamlaka nchi hii zimeshikwa na mashetani. Hivyo wakati wote mashetani hayo yanapanga uovu dhidi ya wanadamu wema.
ZCO ndio nani kwenye Nchi hii ndio mwenye mamlaka ya kuamua nani afe na nani aishi?
 
nani anahujumu 4R
Wamesema ili 4R zifanye kazi inabidi kuwe na R nyingine ya 5 inayochunguza hizo 4R km kweli zinafanya kazi kwa hio 4R hazitoshi inabidi ziwe 5R
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Tatizo NI zaidi ya KATIBA, taja mmoja mmoja kuanzia dada WA pikipik weka picha hapa, au leta list na majina yote ya wafanya matukio, ipo siku kitaeleweka, tuache kulaumu order za wakubwa Bali tumfundishe aliyetekelez order. Kaz gan au pesa gani inakujengea uadui na jamii alafu ukazid kuipenda?.

Au mwanangu, kijana wangu au jirani yangu ..NAMI niitafute chain yako .hata kama unaishi TANAHIMBA. .hata kama wazaz wako WAZEE kiasi gani Toa maumivu kwao. Ndo sasa tutapeleka ujumbe Sawa. Tatizo la kusoma vitu bila ushahid vikome, kama unajua anayetekeleza upuuzi huo make na weka picha na tukio alifanya. Ama dote tuvunke katiba au sote TUESHIMU KATIBA. my blood shed will nourish the tree that will lead to seek the freedom...

Hamna taaluma uliyonayo peke yako hapa DUNIANI hivyo binadam hastahili kuji guarantee uchafu na ubabe Kwa mwingine..Jpm Yuko wap, wako WAPI waliotoa matamka mabovu wakiwa mawekaliq viti bungeni, wako wapo makamishna wa vyombo vya usalama waliooamin wao ndo nchi yenyewe?, wapo WAPI wakimind bila wao nchi itayumba?

Wapo WAPI waliooaminccm ndo kila kitu km kangi lugola na Yule mwenye hicho la ... "intelligence yetu imebaini vitendo vya kiurafu" wapo WAPI waliodhani nchi hii au Chama flani wao ndo wanakisimika kana nnape na Mzee makamba sr?. Siku TZ itapoteza hii doz ya kuamin Kufa ni Sehem ya Maisha PATACHAFUKA SANA. kila MTU apewe adhabu yake Kwa kipimo anachostahili, usimuonee MTU Kwa njaa zako na uelewa mdogo wako....wapo candidates wazur zaidi yako ingawa hawapo kwenye hiyo status unamilik Leo hivyo usijiamini Sana...

JAMII inifunzie kwenye IMANI ya waumin waliooamin KAKOBE NI Bora kuliko nguvu ya umeme, au Moses Korola Leo je Wana wafuasi kuzid MWAMPOSA...?. Jua KESHO unaweza kuwa ya Moto yako au baridi yako. TUESHIMU watu.
 
Hivi kwenye mambo kama haya iweje Rais, Waziri Mkuu, IGP huwa hawazungumzi kwa namna yeyote ile
 
Habari wapendwa, kuna taarifa inatembea mitandaoni kuwa Dkt. Slaa amepata taarifa ya Deusdedit Soka ya kwamba atauawa leo na kutupwa msituni, je, Taarifa hiyo ni kweli imetoka kwa slaa? Na ina ukweli?

Asante sana Jamii Check, this is noble job mnafanya kazi nzuri iliyotukuka, ni Mungu ndio atawalipia.
Mungu Ibariki Tanzania na kuipusha na madhila ya kihivi!.
P
 
Zamani katiba ilikua nzuri sana wakati hamna utekani? Lini katiba ilibadilika haya mambo yakaanza?
labda kwa kua utakua na umri mdogo chalii. suala la kutekana lilianza toka awamu ya 1. mchonga ndiye muasisi wa kutekana na kushikilia watu vizuizini..hawa wa sasa wanaendeleza waliyofundishwa na muasisi wao. ni awamu ya Mwinyi pekee kulikua hakuna huu upuuzi. awamu ya Ben, Jk, Magu, Saa100 zote zilikua na kutekana na kupotezwa. sema awamu hizi zingine ukuaji wa mitandao umerahisisha kufahamika na kusambaa habari za nama hii kwa urahisi.
 
labda kwa kua utakua na umri mdogo chalii. suala la kutekana lilianza toka awamu ya 1. mchonga ndiye muasisi wa kutekana na kushikilia watu vizuizini..hawa wa sasa wanaendeleza waliyofundishwa na muasisi wao. ni awamu ya Mwinyi pekee kulikua hakuna huu upuuzi. awamu ya Ben, Jk, Magu, Saa100 zote zilikua na kutekana na kupotezwa. sema awamu hizi zingine ukuaji wa mitandao umerahisisha kufahamika na kusambaa habari za nama hii kwa urahisi.

Mwinyi Katiba ndo ilimbana?
 
Back
Top Bottom