Linus w slaa
New Member
- Jan 29, 2025
- 4
- 7
Kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo unatarajiwa kusomwa uamuzi juu ya uhalali wa hati ya mashtaka kwenye kesi zinazomkabili mwanasiasa mkongwe nchini Dkt. Wilbroad Slaa.
Dkt. Slaa hajafikishwa mahakamani hapa na sababu iliyoelezwa na upande wa jamhuri kuwa ni uwepo wa changamoto ya usafiri(gari) ambalo lingetakiwa kuwaleta washtakiwa katika mahakama hiyo.
Jibu hilo limetolewa baada ya wakili wa Dkt. Slaa, Peter Madeleka kuhoji juu ya kutofikishwa mahakamani kwa Dkt. Slaa.
Pia soma > Pre GE2025 - Mahakama Kuu yaagiza dhamana ya Dkt. Slaa ishughulikiwe haraka
Kesi ya Dk. Slaa yaendelea bila kuwepo Mahakamani, Wakili wa Jamhuri asema gari lililotakiwa kuleta washtakiwa limepata tatizo la kiufundi
Licha ya Kesi namba 993 ya Mwaka 2025 inayomkabili Dkt. Slaa kutajwa leo Januari 31, 2025 lakini mshtakiwa huyo hajafikishwa Mahakamani kutokana na kilichodaiwa kuwa kumetokea na changamoto ya kiufundi kwenye gari la liliotakiwa kuwaleta watuhumiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Baada ya Mawakili wa Upende wa utetezi wakiongozwa na Wakili Hekima Mwasipu kutaka kufahamu sababu za mteja wao kutolewa Mahakamani, Wakili wa Jamhuri amejibu kwa kusema kwamba kumetokea tatizo la kiufundi kwenye gari ambalo lilitakiwa kuwaleta washtakiwa mahakamani ikiwemo Dkt. Slaa.
Kesi hiyo inaendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ikiwa ni siku moja baada Mahakama Kuu Tanzania, Masijala Kuu Dar es Salaam kuagiza shauri la Dkt. Wilbroad Slaa lirejeshwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake.
Dkt. Slaa kupitia Mawakili wake walifungua shauri la mapitio la kesi yake katika Mahakama Kuu kupinga mwenendo wa Mahakama ya Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa dhamana yake kutokana na maombi ya kupinga dhamana yaliyotolewa na Jamhuri.
Itakumbukwa Dkt. Slaa alikosa dhamana tangu alipofikishwa Mahakamani Januari 10, 2025 kusomewa shtaka linalomkabili la kusambaza taarifa za uongo kupitia Mtandao wa X.