Dkt. Slaa: CHADEMA haikwepeki katika kuamua mustakabali wa Tanzania

Dkt. Slaa: CHADEMA haikwepeki katika kuamua mustakabali wa Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Dr. Wilbrod Slaa amesema CHADEMA ndiyo kinara wa kuongoza katiba mpya kwani ipo frontline na imejibainisha kubeba agenda hii ya muhimu kuliko vyama vyote vilivyosajiliwa Tanzania.

Dr. W. Slaa anaongeza kuwa njama zozote za kuipiku CHADEMA katika jambo la katiba mpya kwa kukiweka chama hiki cha upinzani pembeni ni kulirudisha nyuma taifa.

Nguli huyu wa siasa za tanzania anapigilia msumari kuwa agenda hii isifayiwe hujuma kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya shughuli za siasa ikiwemo mikutano ya kisiasa pia kuwaingiza washika dau muhimu kama azaki za kupigania haki za binadamu, vyama vya wakulima, vyama vya wavuvi, vyama vya wafugaji, vyama vya taaluma za kisheria kuruhusiwa kuwa huru kuchangia kazi kubwa iliyobebwa na kufanywa na CHADEMA mpaka sasa.

CCM ina maslahi na mfumo wa sasa na ndiyo maana imeshindwa kubeba ajenda ya katiba mpya kwa kuonekana wanasuasua kwa kuja na hoja dhaifu huku matendo ya CCM yanaonesha matendo yao ni kufubaza msukumo huu wa kuwepo katiba mpya.

Dk. Slaa afichua kundi kubwa la wabunge CCM mwaka 2015 walitaka kusajili chama cha siasa wakiongozwa na spika, lakini wakagundua hawawezi kusajili chama kipya cha siasa kwa kutumia katiba na sheria mbovu zilizopo zinawabana wakaamua kujiunga na CHADEMA.

Source: Mubashara studio
 
Mbona habari nyingi siku hizi jf zina source # 1 kisha source # 2 na mwishoni zinamalizia na Tunachokijua:?
 
Back
Top Bottom