Dkt. Slaa: CHADEMA haikwepeki katika kuamua mustakabali wa Tanzania

Akili kubwa hujadili hoja akili ya Kati hujadili matukio na akili ya chini hujadili watu "Socrates

Dr Slaa yako sawa [emoji817]% cdm wanatakiwa kubeba agenda ya katiba mpya kwa maslahi ya taifa maana ndani ya ccm kumejaa Chawacracy na Tumbocracy.

"Sio lazima unielewe"
Simple minds discuss people ordinary minds discuss events great minds discuss ideas 👍👍🙏🙏🙏
 
Dr. Wilbrod Slaa amesema CHADEMA ndiyo kinara wa kuongoza katiba mpya kwani ipo frontline na imejibainisha kubeba agenda hii ya muhimu kuliko vyama vyote vilivyosajiliwa Tanzania.

Dr. W. Slaa anaongeza kuwa njama zozote za kuipiku CHADEMA katika jambo la katiba mpya kwa kukiweka chama hiki cha upinzani pembeni ni kulirudisha nyuma taifa.

Nguli huyu wa siasa za tanzania anapigilia msumari kuwa agenda hii isifayiwe hujuma kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya shughuli za siasa ikiwemo mikutano ya kisiasa pia kuwaingiza washika dau muhimu kama azaki za kupigania haki za binadamu, vyama vya wakulima, vyama vya wavuvi, vyama vya wafugaji, vyama vya taaluma za kisheria kuruhusiwa kuwa huru kuchangia kazi kubwa iliyobebwa na kufanywa na CHADEMA mpaka sasa.

CCM ina maslahi na mfumo wa sasa na ndiyo maana imeshindwa kubeba ajenda ya katiba mpya kwa kuonekana wanasuasua kwa kuja na hoja dhaifu huku matendo ya CCM yanaonesha matendo yao ni kufubaza msukumo huu wa kuwepo katiba mpya.

Dk. Slaa afichua kundi kubwa la wabunge CCM mwaka 2015 walitaka kusajili chama cha siasa wakiongozwa na spika, lakini wakagundua hawawezi kusajili chama kipya cha siasa kwa kutumia katiba na sheria mbovu zilizopo zinawabana wakaamua kujiunga na CHADEMA.

Source: Mubashara studio

Hizi story za kutunga hazina maana yoyote, ni wabunge gani wa CCM walijiunga CDM kwa kuletwa na Lowassa?
 
CC: Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom