Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Mkuu kwa nchi hii utawapata wapi?
Kwa Ile ya walioba ililetwa na chama Cha siasa gani?? Narudia Tena iundwe taasisi huru ya watu isiyokuwa na mhemuko wala kuongozwaa na chama chochote Cha kisiasa ijapokuwa washiriki wa mchakato huo huenda wakawa na vyama vyao wavipendavyo. Chama chochote chakisiasa kikiongoza zoezi hili haita patikana katiba ya wananchi matokeo yaki itakuwa katiba Kwa matakwa ya chama hicho. Tutakosea pakubwaa
 
Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na maridhiano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Tena yeye aliunga Juhudi za Marehemu. Hayakuwa maridhiano?
 
Vyama vya siasa vikae kimyaa kabisa kwenye mchakato wa siasa. Kama hoja nikatiba hiii inawaonea wa vyama vya upinzani sio kweli nakukatalia kabisaa, jeee ikitokea wakashinda Kwa katiba hiiii itakuwa ushindi wao ni batiliii?? Mbona wabunge wa upinzani wako bungeni si Kwa katiba hiii hiiii???
 
Narudia Tena iundwe taasisi huru ya watu isiyokuwa na mhemuko wala kuongozwaa na chama chochote Cha kisiasa ijapokuwa washiriki wa mchakato huo huenda wakawa na vyama vyao wavipendavyo..
Kuunda taasisi siyo suluhisho. Tume ya uchaguzi ya akina MAHELA, na ile ya akina JECHA nazo ziliundwa lakini zikakosa tija kabisaa
 
Sahivi kuna udini mkali sn teuzi zote ni Tanga, Pwani na Zanzibar
Tunao uhuru wa kuongea, tunao uhuru wa kufanya nikutano ya kisiasa, hakuna cha watu wasiojulikana, .Sehemu za Ibada zimebakia kwa ajili ya ibada na sio masuala ya kuongelea siasa za chama kimoja .....
 
Yeye kama mtanzania kama walivyo watanzania wengine ,ni Nini mchanga wake au mpango wake nje ya maridhiano kuhakikisha katiba mpya unapatikana?!.
 
Hakuna mwananchi asiye na mrengo wa kisiasa..!!

Wote tuna mrengo kama sio mrengo wa kushoto basi wewe ni wa mrengo wa kulia na kama hauko kotekote huko basi wewe ni wa mrengo wa kati..!

Unaweza ukawa unaishi tu na usilijue lakini huo ndiyo uhalisia..

Na kumbuka hili:

Kila mtu anaathiriwa na siasa. Na ndiyo kusema siasa ndiyo hayo maisha unayoishi. Siasa ndiyo inayoamua upate huduma za kijamii kama maji, umeme, barabara, elimu nk za ubora au uduni wa kiwango gani..

Siasa ndiyo inayoamua wewe Ujamaa ni mhimu uwe na maisha ya kiuchumi ya namna gani. Siasa na wanasiasa ndiyo wanaamua mfumo wa maisha ya kijamii, siasa, utamaduni na uchumi wa watu katika nchi uweje..

Siasa ni mfumo wa maisha ya watu ktk nchi au taifa fulani

Kwa hiyo unaposema "chama chochote cha siasa kiachane na harakati za kutafuta katiba ya wananchi" bila shaka unakuwa hujui unasema nini..!!

Chama cha siasa siyo kitu au kiumbe fulani kisicho na uhai. Chama cha siasa ni watu. Kwa kauli yako hii Ina maana watu wote wafe na maana yake ndiyo inakuwa mwisho wa chama siasa!!!

Unataka katiba ya wananchi, ungana na wananchi wenzako waliokwisha weka wazi misimamo yao kisiasa pengine na vyama vyao vya siasa..!!
 
Wananchikaribia wote wanavyama vyao, ila tunachokataaa, wasitumie vyama vyao kudai katiba ya wananchi. Maana katiba ya wananchi ni Sheria mama, hivyo haitakiwi kubuguziwa na chama chochote Cha kisiasa. Tunavyama vingi vya siasa tukiruhusu vyama hivyo Kila kimoja kiingize umasilahi wake hatuta pata katiba ya wananchi, matokeo yake ni katiba ya matakwa ya watu na vyama vyao. Hivyo iundwe taasisi huru kama ya akina warioba ndio ichakate na kudai katiba ya wananchi, licha ya kuwa hao nao watakuwa na vyama vyao wavipendavyo. Tukirusu makundi ya vyama vya siasa kunajisi mchakato wa katiba hatutaelewana matokeo yake tutamwaga damu. Hivyo ni vyemaa iundwe time huru kabisa ichakate zoezi Hilo, vyama vya siasa vitaalikwa kama wajumbe wengine ilikuchangia maoni Yao. Lakini sio matakwa Yao, na vikubali kwamba so Kila wao wanachokitaka lazima kiwekwe, lazima wakubali kukosolewa Kwa kile wanachokiamini kingewekwa kwenye katiba ya wananchi. Hiii tunataka katiba ya wananchi sio katiba ya chama Cha siasa. Tukitengeneza katiba Kwa mihemko ya vyama vya siasa tutapigana na hatutoelewanaa. Asante.
 
Hao wananchi hawahitaji uongozi?

Juhudi za hao wananchi hazihitaji kuratibiwa?

Wakati mwingine mnajifanya kuwa na akili kichwani kumbe ndani ni patupu kabisa!

Uliona wapi wananchi wakifanya jambo bila ya kuwepo na usimamizi wa kuratibu shughuli zao!

CHADEMA kuwepo kwenye nafasi hiyo haina maana ndiyo inayopigania katiba yao; hii itakuwa ni kazi ya wananchi wenyewe.
 
Itengenezwe tume huru, ndani yake kutakuwa na viongozi kama vile kipindi Cha akina walioba na wenzao. Hao ndio watakao ratibu zoezi, na haoviongozi wa vyama vya siasa watakuwa waalikwa kwma wajumbe wengine. Hujanielewa wapii bwasheee???
 
Itengenezwe tume huru, ndani yake kutakuwa na viongozi kama vile kipindi Cha akina walioba na wenzao. Hao ndio watakao ratibu zoezi, na haoviongozi wa vyama vya siasa watakuwa waalikwa kwma wajumbe wengine. Hujanielewa wapii bwasheee???
Ni nani atakayeweka msukumo wa kufika hatua hiyo kama siyo hao CHADEMA na makundi mengine wanaounganisha juhudi za wananchi kuishinikiza serikali iruhusu mchakato huo?
 
Huyu Mzee wa Kinyaturu ni tofauti sana na Tundu Lissu.

Huyu Mzee ni kigeugeu rahisi kuhongwa na CCM lakini hebu tumpe second chance.

Jana nilikuwa nikimsikiliza alipokuwa akifafanua upigaji wa ardhi uliofanywa na Hussein Bashe Mzee yuko vizuri labda njaa tu ndio zinazomsumbua.
 
Ni nani atakayeweka msukumo wa kufika hatua hiyo kama siyo hao CHADEMA na makundi mengine wanaounganisha juhudi za wananchi kuishinikiza serikali iruhusu mchakato huo?
Ukisha sema chadema kwenye katiba ya wananchi sio sawa nchiii sio chadema pekeee kunavyama vingi. Chadema wataalikwa kama wajumbe wengineee. Kwani tume ya warioba ilihamasishwa na chama kipiii??
 
Huyu Slaa haaminiki tena yeye alishakula mihogo wakati yupo CHADEMA aiache CHADEMA na mambo yake yeye aende Lumumba akachukue mgao wake.
 
Unachoongea hakieleweki. Kuna aliyewazuia hao wananchi ukiwemo wewe kudai katiba mpya? Mbona hatujawaona mkidai huo mchakato? Waacheni Chadema wafanye wanavyoona inafaa. Wakati wanapitishwa kwenye moto kwa suala hilohilo si mlijificha nyuma ya keyboard kuwadhihaki? Leo pressure yao imesaidia walau, halafu mnafiki mmoja anaibuka eti "wananchi ndio wadai katiba". Muone.
 
Hivyo vyama vyenu vipiganie katiba yenu, kama mnataka kupigania katiba ya wananchi jivueni mwamvuli wa chama chenu muonekane neutral hapo mtatafuta katiba ya wananchi. Sawaaa bwasheee.
 
Slaa ni mwanasiasa bora kuwahi kutokea hapa Tanzania. Dr Slaa ni mkubwa kuliko CHADEMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…