Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Vyama vya siasa vikae kimyaa kabisa kwenye mchakato wa siasa. Kama hoja nikatiba hiii inawaonea wa vyama vya upinzani sio kweli nakukatalia kabisaa, jeee ikitokea wakashinda Kwa katiba hiiii itakuwa ushindi wao ni batiliii?? Mbona wabunge wa upinzani wako bungeni si Kwa katiba hiii hiiii???
Mbunge gani halali wa upinzani yuko Bungeni?
 
Naunga mkono hoja Samia amutueweka hostage na Maridhiano yake. Yani Kuna mambo wanakubaliana sirini halafu sisi huku tunalazimishana kuyatii.
Hiyo collaboration ya Samia na Mbowe mtaelewa taratibu tu na hasa wale ambao ndio wanaanza kuzijadili siasa za nchi hii na hawajui ujanja wa CCM na ujue kwa sasa kuna vibe za kinafiki against vibe za ukweli muda ni mwalimu mzuri utaongea.
 
Unampinga mwenyekiti wako
Mwenyekiti wangu hana kosa lolote maana hata alipofirisiwa miradi yake na mashamba yake kwenye awamu ya tano alivumilia,pia amefungwa kwa kesi ya ugaidi na Samiah kavumilia,Ruzuku ni sheria yetu inatamka hivyo wala siyo Mwenyekiti.
 
Naona mzee anatafuta uteuzi kwa nguvu zake zote, Nimegundua kuna watu wakiwa nje ya system wanajiita wapinzani lakin wakipewa cheo wanatulia lakini akitemwa analianzisha upya ili afikiriwe tena.
 
Yan inauzi kweli huyu balozi mst anakuja kufanya usnitch wa kichawi hapa, sijui ndo keshahongwa? Hivi kwa nini asiwanange ccm ambao ndo wanazuia mchakato wa katiba mpya? Kwa nini havisemi vyama vingine na viongozi wao wanafanya nini kuwezesha katiba mpya? Makundi mbalimbali na wananchi wote, akiwemo slaa mwenyewe wanafanya nini? Kwani ni mbowe tu na cdm ndo wanaotaka katiba mpya?
Slaa ana HAKI kuhoji Kwa niaba ya wananchi.

Alipita Nchi nzima kukusanya maoni ya Katiba mpya.
 
Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na maridhiano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Tatizo ni jukwa kwa Sasa slaa Hana jukwaa la kusema haya ndo maana Kila siku anabwatuka tu!
 
Mwenyekiti wangu hana kosa lolote maana hata alipofirisiwa miradi yake na mashamba yake kwenye awamu ya tano alivumilia,pia amefungwa kwa kesi ya ugaidi na Samiah kavumilia,Ruzuku ni sheria yetu inatamka hivyo wala siyo Mwenyekiti.
Gaidi unampinga
 
Slaa ana HAKI kuhoji Kwa niaba ya wananchi.

Alipita Nchi nzima kukusanya maoni ya Katiba mpya.
Kwa hiyo anamuhoji mbowe ndo mwenye katiba mpya? Anataka kusema Mbowe hataki katiba? Kwa nini hazihoji Mamlaka husika? Kwa nini ahihoji ccm ambayo ndo inayozuia mchakato kwa maslahi yao binafsi? Huyo slaa anajua mbowe alikuwa wapi na anafanyiwa nini wakati yeye slaa alivoungana na serikali ya ccm kula mema ya nchi na kuhujumu demokrasia ikiwemo katiba mpya?
 
Kwa hiyo anamuhoji mbowe ndo mwenye katiba mpya? Anataka kusema Mbowe hataki katiba? Kwa nini hazihoji Mamlaka husika? Kwa nini ahihoji ccm ambayo ndo inayozuia mchakato kwa maslahi yao binafsi? Huyo slaa anajua mbowe alikuwa wapi na anafanyiwa nini wakati yeye slaa alivoungana na serikali ya ccm kula mema ya nchi na kuhujumu demokrasia ikiwemo katiba mpya?
HOJA Dr Slaa ni kuwa, kama maridhiano ni Kwa ajili ya Watanzania, haipaswi kuwa SIRI ya vyama viwili.
 
HOJA Dr Slaa ni kuwa, kama maridhiano ni Kwa ajili ya Watanzania, haipaswi kuwa SIRI ya vyama viwili

HOJA Dr Slaa ni kuwa, kama maridhiano ni Kwa ajili ya Watanzania, haipaswi kuwa SIRI ya vyama viwili.
Hiyo hoja unaona ni muafaka kuelekezwa kwa mbowe na mtu kama slaa? Kwa nini asimlenge Rais na ccm ambao ndo wameshikilia karata?
 
Akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii Aprili 20, 2023, Dkt Slaa amesema akipata nafasi ya kukutana na mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe atamshauri aachane na maridhiano kwa kuwa hayafai.


“Nikipata nafasi ya kukutana nitamwambia kwamba fuata principle za siasa safi, simamia, kwa sababu kwa sasa unatakiwa kuwapatia watanzania katiba mpya. Maridhiano hayafai” amesema

Amesisitiza, “Maridhiano hayafai kwasababu yanakaa zaidi ya mwaka, hakuna taarifa kwa wananchi. Maridhiano si mali ya Samia na ya Mbowe. Katiba inayodaiwa ni ya watanzania. Katiba si mali ya watu wawili, wala sio ya CCM na CHADEMA, ni ya watanzania. Watanzania lazima wajue wanataka katiba ya aina gani”
Dkt Slaa amesema amemsikia mara kadhaa Rais Samia akisema kuwa wataangalia katiba ya mwaka 1977 kwa kuwa Rasimu ya Warioba imepitwa na wakati, yeye anasema haya ni makosa makubwa sana.

“Someni preamble pale kwenye katiba mwanzoni imeandikwa nini, imeandikwa sisi watanzania tumeamua, kwenye katiba”

Kuhusu kusubiria uteuzi, amesema kwa umri wake hasubirii tena fursa hiyo, pia amemsfia Freeman Mbowe kuwa mwanasiasa mzuri, mkonge na mpambanaji wa siku nyingi.


Chanzo: East Africa Radio
Mbowe hajaingia tu kwenye maridhiano kwa kutaka. Mbowe ameambiwa, "umetufanya tuonekane wasaliti na waasi ndani ya nchi yetu, serikali na ndani ya chama chama cha mapinduzi, hatuaminiki tena, hatutakiwi tena".
Kwa hiyo FAM hajiwakilishi yeye tu na haiwakilishi chadema tu.
Mbowe ana sababu zingine za kiintelijensia za kukubali kufanya maridhiano na kwa sababu hiyo, Mbowe hatajitoa kwenye maridhiano hata akosolewe na kila mtu.
CCM wao wapo kwenye maridhiano ili
1. Kupunguza kelele na kuwepo kwa political instability.
2. Kuweza management ya public pressure.
 
Wananchikaribia wote wanavyama vyao, ila tunachokataaa, wasitumie vyama vyao kudai katiba ya wananchi.
Unaelewa unazungumza nini lakini? Unaelewa maana ya "chama cha siasa" kweli wewe?

Vyama vya siasa ndiyo hao watu. Utasemaje wafanye shughuli zao nje ya vyama vyao?

Mimi bado naamini huelewi unazungumza nini...!!
Maana katiba ya wananchi ni Sheria mama, hivyo haitakiwi kubuguziwa na chama chochote Cha kisiasa.
Hujui unasema nini wewe. Unahitaji kuelimishwa..!!

Wewe unadhani chama cha siasa ni kitu gani? Ni mlima au mnyama fulani?

Kama ulikuwa hujui, ngoja nikufundishe:

Kwamba, chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu ambaao ndiyo hao wananchi unaowasema. Hawa nao katiba inawahusu na ni ya kwao pia Kwa sababu imebeba maslahi yao kama wananchi..

Muhimu ni makundi yote ya kijamii (all social fractions) kuungana na kuidai hiyo katiba...
Tunavyama vingi vya siasa tukiruhusu vyama hivyo Kila kimoja kiingize umasilahi wake hatuta pata katiba ya wananchi, matokeo yake ni katiba ya matakwa ya watu na vyama vyao.
Ingia na wewe kwenye harakati hizo za kudai katiba mpya ili uhakikishe maslahi yako yanaingia kwenye katiba mpya...

Cha ajabu wewe unataka vyama vya siasa visishiriki. Je, maslahi yao yatawakilishwa na nani kwenye katiba mpya itakayoandikwa?

Kwanini huelewi simple logic kama hii? Umesomea shule gani wewe?
Hivyo iundwe taasisi huru kama ya akina warioba ndio ichakate na kudai katiba ya wananchi, licha ya kuwa hao nao watakuwa na vyama vyao wavipendavyo.
Hapa kidogo akili zimekurudia na umeandika something sensible...

Lakini kabla ya kuundwa hiyo taasisi, lazima wananchi wa makundi yote ya kijamii (ukiwemo wewe bodaboda) mshirikiane na taasisi zingine huru kama vyama vya siasa (CCM, CHADEMA, ACT WAZALENDO, CHAUMA nk); NGOs, vyama vya kitaaluma kama TALGWU, MEWATA, CWT, RAAWU nk; vyama vya wakulima na wafugaji nk nk ili kutia pressure kwa watawala wenye mamlaka ya kisheria kukubali matakwa ya wananchi na kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya..
Tukirusu makundi ya vyama vya siasa kunajisi mchakato wa katiba hatutaelewana matokeo yake tutamwaga damu.
Hakuna unajisi hapo. Ni haki yao pia maana nao ni sehemu ya wananchi wa nchi hii na katiba inawahusu na imebeba maslahi ya kisiasa vile vile...
Hivyo ni vyemaa iundwe time huru kabisa ichakate zoezi Hilo, vyama vya siasa vitaalikwa kama wajumbe wengine ilikuchangia maoni Yao.
Nisome huko☝️☝️☝️☝️huko juu utaelewa
Lakini sio matakwa Yao, na vikubali kwamba so Kila wao wanachokitaka lazima kiwekwe, lazima wakubali kukosolewa Kwa kile wanachokiamini kingewekwa kwenye katiba ya wananchi.
Huelewi. Nisome kuleeeee juu☝️☝️☝️
Hiii tunataka katiba ya wananchi sio katiba ya chama Cha siasa.
Vyama siasa ni vinaundwa na wananchi pia. Nao katiba mpya inawahusu. Unataka waende wapi..?

Hujui unaandika nini!!
Tukitengeneza katiba Kwa mihemko ya vyama vya siasa tutapigana na hatutoelewanaa. Asante.
Katiba mpya inatakiwa ibebe Kila aina ya "mihemko" toka makundi yote ya kijamii kama vile:

1. Wafanyakazi wa sekta ya umma (walimu, madaktari, wahasibu, wanasheria nk)

2. Wakulima & wafugaji..

3. Wanasiasa na vyama vya siasa.

4. Bodaboda, mamantilie, mafundi sherehani nk nk...

WHY? Kwa sababu hawa wote ni wananchi na katiba ni yao!!
Kama utakuwa hujaelewa mpaka hapo, basi wewe utakuwa na roho ngumu kwelikweli..!!

Kwa heri..
 
Back
Top Bottom