Pre GE2025 Dkt. Slaa: Mbowe ajitafakari sana. Ataaibika kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, ametoa rai ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kujitafakari na kuachia nafasi ya uongozi ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya cha viongozi kama Tundu Lissu.

Dkt. Slaa ametoa maoni hayo akizungumzia medani za kisiasa za sasa, akisisitiza kuwa nyakati zimebadilika na zinahitaji mbinu mpya na viongozi wapya wenye uwezo wa kukabiliana na serikali ya CCM kwa ujasiri na ukali wa hoja.

“Kila mtu anatakiwa katika mapambano kwa wakati fulani. Leo si wakati wa Mbowe. Miaka 30 ya uongozi wake imemaliza mchango wake mkubwa, lakini sasa taifa linahitaji watu tofauti kama Lissu na Heche ambao hawamung’unyi maneno,” amesema Dkt. Slaa katika mazungumzo yake ya hivi karibuni.

Akifafanua zaidi, Dkt. Slaa amesema kuwa mbinu za kisiasa zilizofanikiwa chini ya uongozi wa Mbowe hapo awali zimepitwa na wakati. Hii ni kutokana na mabadiliko makubwa katika mfumo wa siasa na ujasiri unaohitajika leo kukabiliana na utawala wa CCM.

Dkt. Slaa amesisitiza kuwa Tanzania ya sasa inahitaji viongozi wenye msimamo mkali na wa moja kwa moja dhidi ya CCM.

“Mbowe ni mtu wa ku-compromise, lakini leo hatuhitaji compromise. Tunahitaji viongozi wa aina ya Lissu na Heche ambao wanaweza kuikemea CCM kwa lugha kali, lakini si ya matusi,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, hotuba za Mbowe za hivi karibuni hazijawahi kuikemea serikali kwa namna ambayo inawapa wananchi ujasiri wa kusimama dhidi ya CCM.

“Mbowe amefanya kazi kubwa kama Musa alivyowatoa waisraeli utumwani. Lakini kama Musa hakuingiza watu wake Kaanani, Mbowe pia anapaswa kukubali kazi hiyo iendelee na kizazi kipya cha viongozi”, amesema Dkt. Slaa.

Tanzania inahitaji viongozi wapya wenye silaha mpya za kisiasa. Mbowe hana uwezo wa kumwondoa Rais Samia madarakani. Tukimung’unya maneno, tutapoteza taifa zima,” amesema.

Dkt. Slaa alikumbushia mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA yaliyofanikisha kupatikana kwa damu mpya katika nyakati tofauti, akiwataja...

SLAA.png

Source: Jambo TV
 
Tatizo Mbowe anawasikiliza wapambe ambao hawafikirii kesho ya Chadema,mtu akisema Mbowe ni Alfa na Omega Chadema huyo ni wa kuogopwa kama ukoma yaani Chadema siyo taasisi bali ni duka la Mbowe watu sampuli ya Yericko na Ntobi wanampoteza Mbowe. Hivi kweli Mbowe hadi sasa hajui wanachama wa Chadema wanataka nini,na kama hajui basi hafai kabisa kuongoza chama tena. Wanachama ambao ndiyo wenye kura za kuweza kuipatia Chadema madiwani na wabunge kuwapuuza ni political suicide. Hao wajumbe 1200 hawawezi kuivusha Chadema.
 
Attachments

  • GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
    GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
    58.9 KB · Views: 5

Mzee huyu anaangqlia Rais dini gani
 
Kushindwa ndio kuaibika?
Kushindwa siyo kuabika, LAKINI kwa mtu uliyefanya mambo mengi, ukapata achievements kadhaa, ukija kuondolewa na watu wale wale bao siku zote walikuunga mkono, inakuwa ni aibu. Hata wewe mwenyewe utabakia unajiuliza maswali mengi.

Kwaajili ya kulinda record yake, Mbowe alitakiwa kuondoka kwa heshima siyo kusubiri aondolewe.
 
Padre baaana! "Nimestaafu siasa" 😆😆
Usimpa dikozoe maneno. Dr. Slaa hajawahi kusema kuwa amestaafu siasa BALI alisema anastaafu siasa za vyama na kubakia kwenye siasa za kitaifa zenye tija kwa nchi". Lakini hata akirudi kwenye siasa za vyama, hafanyi kosa lolote. Kwa kawaida mtu hufanya maamuzi fulani kwa kutegemea mazingira ya wakati huo. Mazingira yakibadilika, mtu ambaye ni dyanamic anatakiwa kubadilika ili kukabiliana na mabadiliko.
 
Kushindwa siyo kuabika, LAKINI kwa mtu uliyefanya mambo mengi, ukapata achievements kadhaa, ukija kuondolewa na watu wale wale bao siku zote walikuunga mkono, inakuwa ni aibu. Hata wewe mwenyewe utabakia unajiuliza maswali mengi.

Kwaajili ya kulinda record yake, Mbowe alitakiwa kuondoka kwa heshima siyo kusubiri aondolewe.
Hakuna aibu yeyote hapo ,wenye njaa ndio wataona aibu na sio Mbowe.
 
Tatizo Mbowe anawasikiliza wapambe ambao hawafikirii kesho ya Chadema,mtu akisema Mbowe ni Alfa na Omega Chadema huyo ni wa kuogopwa kama ukoma yaani Chadema siyo taasisi bali ni duka la Mbowe watu sampuli ya Yericko na Ntobi wanampoteza Mbowe. Hivi kweli Mbowe hadi sasa hajui wanachama wa Chadema wanataka nini,na kama hajui basi hafai kabisa kuongoza chama tena. Wanachama ambao ndiyo wenye kura za kuweza kuipatia Chadema madiwani na wabunge kuwapuuza ni political suicide. Hao wajumbe 1200 hawawezi kuivusha Chadema.
Hasa Yericko sijui ni mwanaccm aliyejificha?
 
Usimpa dikozoe maneno. Dr. Slaa hajawahi kusema kuwa amestaafu siasa BALI alisema anastaafu siasa za vyama na kubakia kwenye siasa za kitaifa zenye tija kwa nchi". Lakini hata akirudi kwenye siasa za vyama, hafanyi kosa lolote. Kwa kawaida mtu hufanya maamuzi fulani kwa kutegemea mazingira ya wakati huo. Mazingira yakibadilika, mtu ambaye ni dyanamic anatakiwa kubadilika ili kukabiliana na mabadiliko.
Hata makocha na wachezaji wa soka hustaafu lakini muda ukiwaruhusu hurudi mchezoni kuendeleza mapambano.
 
Sio sahihi kusema Mbowe ataaibika, hii ni demokrasia, akikosa kura it's okay na maisha yataendelea. Kutumia neno kuaibika, ni kupoteza maana halisi ya demokrasia na kujenga dhana ya watu kutokukubali kushindwa
 
Back
Top Bottom