Pre GE2025 Dkt. Slaa: Mbowe ajitafakari sana. Ataaibika kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, ametoa rai ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kujitafakari na kuachia nafasi ya uongozi ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya cha viongozi kama Tundu Lissu.

Dkt. Slaa ametoa maoni hayo akizungumzia medani za kisiasa za sasa, akisisitiza kuwa nyakati zimebadilika na zinahitaji mbinu mpya na viongozi wapya wenye uwezo wa kukabiliana na serikali ya CCM kwa ujasiri na ukali wa hoja.

“Kila mtu anatakiwa katika mapambano kwa wakati fulani. Leo si wakati wa Mbowe. Miaka 30 ya uongozi wake imemaliza mchango wake mkubwa, lakini sasa taifa linahitaji watu tofauti kama Lissu na Heche ambao hawamung’unyi maneno,” amesema Dkt. Slaa katika mazungumzo yake ya hivi karibuni.

Akifafanua zaidi, Dkt. Slaa amesema kuwa mbinu za kisiasa zilizofanikiwa chini ya uongozi wa Mbowe hapo awali zimepitwa na wakati. Hii ni kutokana na mabadiliko makubwa katika mfumo wa siasa na ujasiri unaohitajika leo kukabiliana na utawala wa CCM.

Dkt. Slaa amesisitiza kuwa Tanzania ya sasa inahitaji viongozi wenye msimamo mkali na wa moja kwa moja dhidi ya CCM.

“Mbowe ni mtu wa ku-compromise, lakini leo hatuhitaji compromise. Tunahitaji viongozi wa aina ya Lissu na Heche ambao wanaweza kuikemea CCM kwa lugha kali, lakini si ya matusi,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, hotuba za Mbowe za hivi karibuni hazijawahi kuikemea serikali kwa namna ambayo inawapa wananchi ujasiri wa kusimama dhidi ya CCM.

“Mbowe amefanya kazi kubwa kama Musa alivyowatoa waisraeli utumwani. Lakini kama Musa hakuingiza watu wake Kaanani, Mbowe pia anapaswa kukubali kazi hiyo iendelee na kizazi kipya cha viongozi”, amesema Dkt. Slaa.

Tanzania inahitaji viongozi wapya wenye silaha mpya za kisiasa. Mbowe hana uwezo wa kumwondoa Rais Samia madarakani. Tukimung’unya maneno, tutapoteza taifa zima,” amesema.

Dkt. Slaa alikumbushia mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA yaliyofanikisha kupatikana kwa damu mpya katika nyakati tofauti, akiwataja...

Source: Jambo TV
kwahiyo mzee slaa kaona ameongea point ya maana sana ee, dah 🐒
 
Dr Slaa ni hawara wa Covid19 anayeitwa Cecilia... ni mzee mwenye tabia chafu sana ya uzinzi. Huyo Cecy ni binti wa aliyekuwa rafiki wa karibu sana wa Dr Slaa yaani walikuwa wale marafiki kama ndugu. Cecy ni kama binti yake. Cha kushangaza Slaa bila aibu akaanza kula tunda kabla hata halijaiva. Pamoja na kurudia mtihani wa form four kwa miaka mingi ila kilaza Cecy aliweza kuupata ubunge viti maalum kupitia Slaa. Ikumbukwe Cecy alimaliza form four 1999 ila hadi 2004 alikua anarudia mtihani.

Kwa maelezo hayo itoshe kusema Slaa hana uhalali wa kimaadili wala kisiasa kumnyooshea Mbowe kidole. Lissu ni adui tu wa demokrasia ila hana skendo nyingi za kimaadili.
 
Tatizo Mbowe anawasikiliza wapambe ambao hawafikirii kesho ya Chadema,mtu akisema Mbowe ni Alfa na Omega Chadema huyo ni wa kuogopwa kama ukoma yaani Chadema siyo taasisi bali ni duka la Mbowe watu sampuli ya Yericko na Ntobi wanampoteza Mbowe. Hivi kweli Mbowe hadi sasa hajui wanachama wa Chadema wanataka nini,na kama hajui basi hafai kabisa kuongoza chama tena. Wanachama ambao ndiyo wenye kura za kuweza kuipatia Chadema madiwani na wabunge kuwapuuza ni political suicide. Hao wajumbe 1200 hawawezi kuivusha Chadema.
Mbowe anashauriwa na Yeriko ni hatari sn
 
Hivi mbowe hawezi kusema kwa maslahi ya mapana ya chama naachia ngazi na sitagombea kupisha mawazo mapya? Mzee Biden alijiondoa kuwania tena urais wa marekani dakika za mwisho na kumuachia mwanamama Kamala Harris aliyeshindwa na ndugu Tramp

kwanini munamuogpa sana mwamaba? kama munajiamini tusibiri sanduku la kura
 
Tatizo Mbowe anawasikiliza wapambe ambao hawafikirii kesho ya Chadema,mtu akisema Mbowe ni Alfa na Omega Chadema huyo ni wa kuogopwa kama ukoma yaani Chadema siyo taasisi bali ni duka la Mbowe watu sampuli ya Yericko na Ntobi wanampoteza Mbowe. Hivi kweli Mbowe hadi sasa hajui wanachama wa Chadema wanataka nini,na kama hajui basi hafai kabisa kuongoza chama tena. Wanachama ambao ndiyo wenye kura za kuweza kuipatia Chadema madiwani na wabunge kuwapuuza ni political suicide. Hao wajumbe 1200 hawawezi kuivusha Chadema.
Mkuu hii picha ya muiba nyuzi za humu usiiweke tena maana mtu anaweza kuipigiza simu yake chini kwa kudhani anamuua.
 
Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, ametoa rai ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kujitafakari na kuachia nafasi ya uongozi ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya cha viongozi kama Tundu Lissu.

Dkt. Slaa ametoa maoni hayo akizungumzia medani za kisiasa za sasa, akisisitiza kuwa nyakati zimebadilika na zinahitaji mbinu mpya na viongozi wapya wenye uwezo wa kukabiliana na serikali ya CCM kwa ujasiri na ukali wa hoja.

“Kila mtu anatakiwa katika mapambano kwa wakati fulani. Leo si wakati wa Mbowe. Miaka 30 ya uongozi wake imemaliza mchango wake mkubwa, lakini sasa taifa linahitaji watu tofauti kama Lissu na Heche ambao hawamung’unyi maneno,” amesema Dkt. Slaa katika mazungumzo yake ya hivi karibuni.

Akifafanua zaidi, Dkt. Slaa amesema kuwa mbinu za kisiasa zilizofanikiwa chini ya uongozi wa Mbowe hapo awali zimepitwa na wakati. Hii ni kutokana na mabadiliko makubwa katika mfumo wa siasa na ujasiri unaohitajika leo kukabiliana na utawala wa CCM.

Dkt. Slaa amesisitiza kuwa Tanzania ya sasa inahitaji viongozi wenye msimamo mkali na wa moja kwa moja dhidi ya CCM.

“Mbowe ni mtu wa ku-compromise, lakini leo hatuhitaji compromise. Tunahitaji viongozi wa aina ya Lissu na Heche ambao wanaweza kuikemea CCM kwa lugha kali, lakini si ya matusi,” amesema.

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, hotuba za Mbowe za hivi karibuni hazijawahi kuikemea serikali kwa namna ambayo inawapa wananchi ujasiri wa kusimama dhidi ya CCM.

“Mbowe amefanya kazi kubwa kama Musa alivyowatoa waisraeli utumwani. Lakini kama Musa hakuingiza watu wake Kaanani, Mbowe pia anapaswa kukubali kazi hiyo iendelee na kizazi kipya cha viongozi”, amesema Dkt. Slaa.

Tanzania inahitaji viongozi wapya wenye silaha mpya za kisiasa. Mbowe hana uwezo wa kumwondoa Rais Samia madarakani. Tukimung’unya maneno, tutapoteza taifa zima,” amesema.

Dkt. Slaa alikumbushia mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA yaliyofanikisha kupatikana kwa damu mpya katika nyakati tofauti, akiwataja...

Source: Jambo TV
Kushindwa uchaguzi na kukubali matokeo ni heshima kubwa na legacy nzuri.

"Janja yake paka panya kwisa gundua' msemo mmoja wa zamani.
 
Dr.Slaa kaa pembeni uangalie viongozi wakichaguliwa kupitia sanduku la kura.
Kwanini unatoa ushauri wa mgombea Mbowe ajiondoe na ili iwe nini?

Hakuna nafasi ya Mwenyekiti kupitia mlango wa nyuma,wala nafasi ya kuvunja katiba ili fulani apewe wenyekiti wa mezani.

Ukiwasikiliza team Lissu kwanza wanadai Mwenyekiti Mbowe ame OVERSTAY kwenye wadhifa wa Uwenyekiti lakini wapo tiyari kwenda uchanguzi. Kwanini hawashindikizi kukarabati katiba kwanza kuweka ukomo wa uwenyekiti ndio uchanguzi ufanyike?

Hata kabla ya vikao rasmi Lissu aishatangaza kugombea uwenyekiti katika mazingira yale yale.
Na mkishindwa mtamulaumu nani?
Haya mambo ya kukalili eti Mbowe must go, bila Effort ya kutatua tatizo kisayansi ni shida.

Ninasapoti ushauri wa Dr. Slaa.
 
Usimpa dikozoe maneno. Dr. Slaa hajawahi kusema kuwa amestaafu siasa BALI alisema anastaafu siasa za vyama na kubakia kwenye siasa za kitaifa zenye tija kwa nchi". Lakini hata akirudi kwenye siasa za vyama, hafanyi kosa lolote. Kwa kawaida mtu hufanya maamuzi fulani kwa kutegemea mazingira ya wakati huo. Mazingira yakibadilika, mtu ambaye ni dyanamic anatakiwa kubadilika ili kukabiliana na mabadiliko.
According to Lissu alipohojiwa na radio moja ya Ulaya wakati ule Slaa alipoiacha CHADEMA mwaka 2015, Lissu alisema Slaa aliporudi nyumbani alitupiwa virago vyake na mchumba wake kwa kukubali Lowassa agombee urais,; hio ndiyo sababu iliyomfanya Slaa astaafu siasa za vyama ili kunusuru uhawara wake na huyo mchumba wake; hata hivyo waliishaachana huko ulaya hivyo Slaa anerudia ubachela.

Hapa nilikuwa nakuhabarisha sababu ya Slaa kuacha siasa za vyama maana naona hujui.
 
Back
Top Bottom