View attachment 3141594
Huyu ndiye John Heche kijana anayetajwa kumrirhi Freeman Mbowe Uenyekiti.
Kwa zaidi au karibu sawa na asilimia 90 ya wananchama na Viongozi wote wanaoondoka chama kikuu cha Upinzani nchi Tanzania Cha CHADEMA hurusha lawama zao kwa Mwenyekiti wa chama hicho anayemaliza muda wake Bw Freeman Aikael Mbowe.
Wakati mmoja aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza la Wanawake la chama hicho Mhe Halima James Mdee toka muungano wa Covid -19 aliwahi kukaririwa Waziwazi akisema walichokifanya yeye na wenzake 18 kina baraka za Mwenyekiti wao huyo Bw Freeman Mbowe.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati kuu wenye misimamo mikali akiwemo John Heche, Tundu Lissu na John Mnyika walionesha dhamira yao ya kutokuwasamehe kabisa wabunge hao 19 wa kike kwa kile walichokifanyia chama hicho chenye ushawishi kwa vijana na Mafukara wa Taifa hilo.
Mwananchi mmoja aliyegoma kutajwa jina lake aliye karibu na Wafuasi wa Mwanasiasa huyo kipenzi cha Watanzania anayedhaniwa kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti wa Taifa ili kumkabili vikali Mwenyekiti wa muda mrefu wa Chama hicho Bw Freeman Mbowe ambae ni mwanasiasa wa muda mrefu endapo tu atagoma kuondoka kwa heshima, Wafuasi wa John Heche wamejinasibu kufungua milango ya msamaha kwa mwanachama na kiongozi yeyote mwenye nia ya kurejea CHADEMA kufanya hivyo bila masharti pindi kiongozi wao huyo atakaposhika udhibiti wa Chama hicho mapema mwezi ujao.
Wafuasi wa Heche wanaona kama kitendo Cha wabunge 19 kukaidi maelekezo ya Chama ni kiashiria cha uongozi dhaifu na uswaiba wa Freeman Mbowe na hivyo kuwapoteza wanawake hao ni kukidhoofisha chama hicho kwani hata Edward Lowassa pamoja na usaliti wake mkubwa kwa Chama chake bado alipokelewa CCM Kwa nderemo na vifijo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli.
Kama kweli Heche atagombea nafasi hiyo na kushinda basi CHADEMA itakuwa ndio chama hatari zaidi Cha Upinzani kusini mwajangwa la Sahara kinachonyemelea dola kwa karibu zaidi kwenye chaguzi zote zinazofuata.
Pia soma Kwanini kila anayeondoka CHADEMA anamtaja Mbowe?