End of day sioni ushindi kwa tunaipinga na wanaounga mkono, ila natumaini CCM na serikali kwa ujumla watakua wamepata somo jinsi gani wananchi walivyo kwa sasa, kwamba nyakati za nguvu ya uma kushika hatamu sio mbali kutoka sasa.
Nguvu ya Umma?! Kutoka kwa umma upi? Sisi hawa hawa wabongo? Mission yoyote ya Kiafrika kufanikiwa mpaka iwe backed up na "mabwana zetu" wa magharibi kwa maslahi yao.
DPW huwa hawashindwi, Watawezesha kukamatwa kwa the so called viongozi wa Sauti ya Wananchi woote, mawakili wote walio frontline, n.k. Waarabu wanachotaka ni Bandari tuu! Utakaa una-argue na watu wapumbavu tusiojitambua Watz?
Nchi yetu na nyingine za Afrika (Zisizojitambua) ipo ktk hatua za mwisho kabisa kuingia kwenye Mfumo wa ubepari kamili. Viongozi wetu ni wajasiriasiasa, wanalijua hilo, hivyo, wanajiandaa kwa kufanya uwekezaji binafsi ili Mfumo uje uwa-accommodate; wanakwiba pesa, wanachukuwa mabilioni ya rushwa kutoka DPW ili waanzishe makampuni ya usafirishaji ya baharini, nchi kavu na angani, wanunue ardhi kwa ajili ya kujenga Bandari za Nchi kavu, kujenga majumba ya kupangisha, n.k. hivyo, wao na vizazi vyao wataushikilia uchumi wa Nchi na watakuwa matajiri milele. Marekani ilikuwa hivyo, Europe ilikuwa hivyo, Urusi ilikuwa hivyo, n.k. Kwa mfano, Urusi ilipokuwa ikiingia kwenye kipindi kama hiki, watawala walifisadi mali za umma isivyo kawaida, wakajilimbikizia ukwasi wa kutisha, waka-invest hadi nje ya Urusi wakinunua makampuni ya biashara barani Ulaya, klabu za soka, n.k.
Tukubali yaishe la sivyo shinikizo la moyo, bp, litatumaliza. Tusio na fursa ya kuwa ktk daraja la watawala tuwe wapole na tuwaandae vizazi vyetu vijavyo kwa ajili ya kutumikishwa na watawala hawa ambao ndio watakuwa mabilionea wameushika na wanauendesha uchumi wa Tanzania kwa kushirikiana na makampuni wawekezaji kutoka nje kama DPW. Hakuna namna.
Kwa Wakristo, tunapoyaona haya, tunainua mioyo na macho yetu kutazama Mbinguni kwani Wokovu wetu uko karibu. Believe me or not.